KATIBU MKUU MAKONDO, UNICEF WAJADILI NAMNA YA KUIMARISHA ULINZI WA HAKI ZA MTOTO


 


 XXXXXXXXXXXXXX

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amekutana na ujumbe wa wawakilishi kutoka UNICEF ukiongozwa na Mkuu wa Ulinzi wa Mtoto, Bi. Maud Droogleever Fortuijn na kujadili namna watakavyoshirikiana  kuimarisha ulinzi wa haki kwa mtoto.

 Bi. Makondo amewahakikishia UNICEF kuwa Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa, 

Aidha ameahidi kuwa wadau watashirikishwa katika hatua zote za maboresho ya mfumo wa haki jinai.

 Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Julai, 2022.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA