KISWAHILI KINAFANYA MAHAKAMA KUTEMBEA ‘KIFUA MBELE’


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokea maandamano ambayo yanahusu Kiswahili na haki kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Utamaduni Duniani (MASIKIDU). 

 



Maandamano yakipita mbele ya Waziri Ndumbaro.

 XXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mwelekeo wa Serikali katika kukiendeleza Kiswahili unafanya Mahakama kutembea ‘kifua mbele’ kwa kuzingatia usemi wa “Thamini chako”. 

 

Mhe. Ndumbaro amesema hayo Julai 4, 2022 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam wakati anapokea maandamano ambayo yanahusu Kiswahili na haki kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Utamaduni Duniani (MASIKIDU). 

 

“Kiswahili chetu tu, ndicho tunachopaswa kujivunia kila siku, lugha za wengine siyo zetu. Kwa hiyo, Kiswahili ndiyo lugha pekee ambayo imetufanya Watanzania kwa miaka sitini ya uhuru, kuishi pamoja na kufanya shughuli zetu kwa undugu, utulivu, amani na umoja.

 

Hatua hiyo imekifanya Kiswahili kupigiwa upatu kitumike katika masuala yote ya kisheria ikiwa ni pamoja na kanuni zake zote ambapo Mahakama ya Tanzania ikiwa mdau wa Kiswahili wanaamini uamuzi unaofanywa na serikali ni wa kizalendo na utawawezesha Watanzania na wananchi kupata fursa za kushiriki katika shughuli za ukalimani, tafsiri, uhariri, uandishi na uchapishaji wa vitabu vya sheria kwa Kiswahili.

 

Hizi ni jitihada za kuwawezesha wananchi kupata haki zao za kuelewa kinachoamriwa na kuandikwa katika michakato ya uendeshaji wa mashauri kuanzia ngazi za mabaraza ya usuluhishi hadi mahakama za juu.

 

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameigiza Wizara ya Katiba na Sheria kushirikiana na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) kuendelea kutafsiri Sheria na Kanuni zote kwa Kiswahili ili wananchi wawawe na nafasi ya kupata uelewa wa mwenendo wa kesi zao na hatua inayosaidia kupata haki zao bila kumwonea mtu.  

 

Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Mahakama za Tanzania utaratibu wa kuwa Mahakama za kimtandao na kutafuta programu ya akili bandia ambao ni mfumo wa kutafsiri na kuandika taarifa za mashauri mahakamani kwenye lugha zaidi ya kumi ikiwamo lugha ya Kiswahili.

 

Zaidi ya hayo, amesema Programu hiyo itakuwa na hatimiliki ya modeli ya Kiswahili na itakuwa chini ya Mahakama ya Tanzania ili Mahakama zingine duniani zikitaka kutumia, lazima wapate kibali cha Mahakama ya Tanzania na walipe tozo ya leseni ambayo ni chanzo cha mapato kwa Serikali.

 

Naye Katibu Mtendaji wa BAKITA Bi. Consolata Mushi amesema kuwa Tanzania ndiyo asili ya Kiswahili ambapo Kiswahili kinatumika kutoka kunakucha hadi kunakuchwa, watu wanaitumia lugha hiyo katika kutekeleza majukumu yao kitaifa, kiuchumi, kijamii na kisiasa.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA