MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YAWE ENDELEVU - WAZIRI NDUMBARO


 


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX



Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) , Waziri wa Katiba na Sheria amesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanatakiwa kuwa endelevu.

Dkt. Ndumbaro amesema hayo kwa niaba ya Mhe. George Simbachachene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) wakati akimkaribisha Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufunga rasmi maadhimsho ya kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika tarehe 1-2 Julai, 2022 Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

"Dawa za kulevya zina madhara makubwa kwa ustawi wa jamii, Maendeleo ya Nchi na Dunia kwa ujumla, hivyo mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya yanatakiwa kuwa endelevu" alisema Dkt. Ndumbaro.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA