SERIKALI YAZUNGUMZA NA WATAALAM WA HAKI ZA BINADAMU (SPECIAL RAPPORTEURS) WA UMOJA WA MATAIFA
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas
Ndumbaro ameongoza kikao na Wataalam wa Haki za Binadamu (Special Rapporteurs)
wa Umoja wa Mataifa wanaoshughulikia masuala ya watu asilia (indigenous people)
na makazi.
Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kawaalika nchini
Tanzania wataalam hao wa haki za binadamu
"kwa niaba ya Serikali nawakaribisha sana
mje kutembelea Tanzania na mpate fursa ya kujionea vivutio vya utalii, tamaduni
zetu na utofauti wa mila mbalimbali za makabila zaidi ya 100 yaliyopo
Tanzania" alisema Dkt. Ndumbaro
Wataalam hao wamepongeza jitihada za Serikali
katika kutekeleza haki za binadamu hususani fidia waliyowapatia waliokuwa
wakazi wa Ngorongoro na kuhamia Msomera wilayani Handeni kwa hiyari yao. Aidha,
wameahidi ushirikiano zaidi na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali
yanayohusu haki za binadamu.
Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao
tarehe 8 Julai, 2022 jijini Arusha, ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka pamoja na watendaji kutoka
Wizara ya Maliasili na Utalii na watendaji kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.
Comments
Post a Comment