WANANCHI MSISUBIRI MATUKIO YA KITAIFA PEKEE KUTAFUTA HUDUMA KWANI VYETI VYA KUZALIWA VINATOLEWA SIKU ZOTE- WAZIRI NDUMBARO
XXXXXXXXXXXXXXXXX
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas
Ndumbaro leo tarehe 6 Julai ,2022 ametembelea na kukagua zoezi la usajili na
kuwapatia vyeti vya kuzaliwa Wananchi linaloendelea katika viwanja vya Maonesho
ya biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Akiongea na Wananchi waliokuwa wakipatiwa
huduma hiyo Mhe, Dkt Ndumbaro amewataka kuwa mabalozi watakaporudi majumbani
mwao Kwa kuwaeleza ndugu, jamaa na majirani zao kuhusu umuhimu wa kusajili
amatukio ya vizazi na vifo, ndoa na talaka na mengineyo kwa wakati badala ya
kusubiri maonesho au matukio yanayowakusanya kwa mwaka mara moja.
‘’Sasa hivi huduma zimesogezwa karibu
yenu kwa upande wa watoto wa umri chini ya miaka mitano wanasajiliwa katika
ofisi za kata na vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika Mikoa
23 na kwa upande wenu watu wazima unaweza kujisajili kielektroniki sehemu
yoyote ulipo Kisha ukapata cheti chako Kwa wakati muafaka’’ Alisema Mhe. Dkt
Ndumbaro.
Kwa upande wake Kabidhi Wasii Mkuu na
Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Angela Anatory amesema mwitikio ni mkubwa wa wananchi
wanaofika kupatiwa huduma ya usajili ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa hivyo
kuwatoa Wasiwasi Kwa kuwa watoa huduma wamejipanga kuhakikisha kila mwenye sifa
ya kusajiliwa anapatiwa huduma hiyo.
‘’Wananchi wamejitokeza na
nimezungumza na baadhi yao wamepongeza na yapo maeneo yenye changamoto
tumeyachukiwa na tutayafanyia kazi Kwa haraka, nashukuru tangu tulipoanza
tarehe 29 Juni, 2022 hadi leo tarehe 6 Julai,2022 tumesajili Wananchi 3,000 na
idadi hiyo itaongezeka kwani wananchi wanaendelea kupatiwa huduma huyo’’.
Alisema Bi. Anatory.
Comments
Post a Comment