WAZIRI NDUMBARO ATETA NA KAMISHNA MKUU WA HAKI ZA BINADAMU WA UN


 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amefanya mazungumzo na Bi. Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo kutolea ufafanuzi tuhuma kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na Hifadhi ya  Ngorongoro.  Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 15 Julai 2022, Geneva Uswisi.

Kwa upande wake, Bi. Bachelet ameshukuru na kupongeza kwa namna ambavyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza masuala ya haki za binadamu hususan chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika mkutano huo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva na Mhe. Hoyce Temu, Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Geneva.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA