WAZIRI NDUMBARO AZURU OFISI YA MASHTAKA NJOMBE

XXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro(Mb), ametembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Njombe akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu tarehe 18 Agosti 2022. Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro amewaasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu. Aidha, Dkt. Ndumbaro ameainisha kuwa jitihada zinaendelea ili kuiwezesha Ofisi hiyo kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kwa kuona namna ya kuongeza bajeti kwa mwaka wa fedha ujao na kuendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali. Dkt. Ndumbaro amekutana pia na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ambapo wamepata wasaa wa kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo haki jinai na utoaji haki kwa ujumla