Posts

Showing posts from August, 2022

WAZIRI NDUMBARO AZURU OFISI YA MASHTAKA NJOMBE

Image
 XXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro(Mb), ametembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Njombe akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu tarehe 18 Agosti 2022.   Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro amewaasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu.   Aidha, Dkt. Ndumbaro ameainisha kuwa jitihada zinaendelea ili kuiwezesha Ofisi hiyo kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kwa kuona namna ya kuongeza bajeti kwa mwaka wa fedha ujao na kuendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali.   Dkt. Ndumbaro amekutana pia na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ambapo wamepata wasaa wa kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo haki jinai na utoaji haki kwa ujumla  

NAIBU WAZIRI PINDA AKABIDHI VIFAA VYA KUENDESHEA MAHAKAMA MTANDAO

Image
 XXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amekabidhi vifaa mbali mbali vya kuendeshea Mahakama mtandao  tarehe 18 Agosti, 2022 katika gereza la mahabusu Wilayani Mpanda.    Vifaa hivyo ambavyo ni Kompyuta mpakato (Laptop) Luninga, Kamera na vingine, vitatumika kuendeshea Mahakama mtandao, ili kuweza kutatua kesi mbalimbali pamoja na kupunguza idadi kubwa ya mahabusu walioko katika gereza hilo.   Akiongea na maafisa wa gereza hilo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mhe. Pinda amesema dhamira ya Serikali ni kuondoa mlundikano wa mahabusu katika Magereza zetu.   Aidha, Mhe. Pinda amemuagiza DPP wa Mkoa wa Katavi ndugu Abel Mwandalama  kuondoa kesi zisizo na mashiko Ili kuondoa mlundikano wa mahabusu kwenye gereza hilo.    Mhe. Pinda amemuagiza DPP kuhakisha kesi zinaendeshwa kwa weledi na kwa kuzingatia haki pamoja na kufanya upelelezi kwa wakati.   Mheshimiwa Pinda amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni tisa kwa ajili ya

WAZIRI NDUMBARO AKUTANA NA DKT. BAERBEL

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Ujerumani Mhe. Dkt. Baerbel Kofler. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu pamoja na wataalam kutoka Ubalozi wa Ujerumani.   Naibu Waziri wa Ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Ujerumani Mhe. Dkt. Baerbel Kofler akifafanua jambo. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Ujerumani Mhe. Dkt. Baerbel Kofler (hayupo pichani).

WAZIRI NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NIGERIA NCHINI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Hamisu Umar Takalamawa. Aidha, mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu pamoja na wataalam kutoka Ubalozi wa Nigeria.

WAZIRI NDUMBARO AKUTANA NA BODI YA TAIFA YA USHAURI WA MSAADA WA KISHERIA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Bodi ya Taifa ya Ushauri wa Msaada wa Kisheria  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. dkt. Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Taifa ya Ushauri wa Msaada wa Kisheria.

WAZIRI NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CANADA

Image
  XXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnell ambaye amefika kumuaga akitarajia kumaliza muda wake wa utumishi mwishoni mwa mwezi Agosti 2022.   Maeneo waliyozungumzia ni pamoja na kubadilishana ujuzi katika ulinzi wa mali asilia, masuala ya haki za binadamu hususani ulinzi kwa watoto, mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, mchakato wa kurekebisha sheria ya ndoa na sheria zinazohusu ushiriki wa wanawake katika siasa.

MABORESHO YA SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

Image
 XXXXXXXXXX Wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wamekutana na kuanza kujadili Sheria ya Huduma za Msaada wa Kisheria, ili kuainisha maeneo yanayohitaji kuboreshwa. Kikao kazi hicho kinaongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria na Msajili wa huduma hizo, Bi. Felistas Mushi na kinafanyika Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 09/08/2022 kwa ufadhili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu-LHRC. 

ZAIDI YA WANANCHI 200 WAPATA ELIMU YA MASUALA YA SHERIA KWENYE MAONESHO YA NANENANE MBEYA.

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXXXX Mamia ya wahudhuriaji wamefurahishwa na Banda la Wizara ya Katiba na Sheria kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.   Maonesho ya Nanenane Mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo; agenda 10/30 Kilimo ni biashara; jiandae kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.    Wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye Banda la Wizara ya Katiba na Sheria wamepata wasaa wa kujifunza na kuuliza maswali mbalimbali hasa kuhusu sheria ya ndoa, ya ardhi, mirathi na sheria ya mtoto.   Zaidi ya wananchi 200 wamepatiwa elimu na ushauri wa Kisheria.   Aidha, suala la mirathi ndio limekuwa likiulizwa Kwa wingi na wananchi kupatiwa ufafanuzi na maelekezo ya kuweza kutatua tatizo hilo.   Maonesho haya yamefungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agosti, 08, 2022.  

MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA 2022.

Image
  Wananchi wa mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya na vitongoji vyake wametembelea kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria kupata elimu  ya masuala ya Sheria ikiwemo Katiba, Haki za Binadamu, Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi na Huduma ya Msaada wa Kisheria. Wakili wa Serikali Mkuu Lawrence Kabigi ametoa huduma hiyo leo  Agosti 06, 2022 katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA 400 MAJIMAJI SELEBUKA 2022, 81 WAKIPATIWA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA.

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXX Wizara ya Katiba na Sheria imetoa huduma kwa wananchi zaidi ya 400 katika Tamasha la Majimaji Selebuka lililomalizika leo 30 Julai, 2022 wilayani Songea-Ruvuma.   Akifunga Tamasha hilo Mbunge wa Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushiriki na kutoa huduma katika Tamasha hilo.   “Natoa pongezi kwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ushiriki wenu na huduma za msaada wa kisheria mliotoa kwa wananchi waliofika kuwatembelea" alisema Dkt. Ndumbaro.   Katika tamasha hili lililoanza tarehe 23 Julai, Wizara kwa kushirikiana na watoa huduma za msaada wa kisheria (paralegals) wametoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi 81 wilayani Songea.   Aidha, nakala 270 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vipeperushi mbalimbali vya sheria ya ndoa, mtoto, mirathi na ardhi vimegawiwa bure kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara.  

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. GEOPHREY PINDA AWATAKA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA KUTOKIUKA KANUNI

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geophrey Pinda akihutubia wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mkoa wa Ruvuma, leo tarehe 29 Julai 2022.   . Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria, Bibi. Mary Makondo akizungumza na watoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mkoa wa Ruvuma kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, leo tarehe 29 Julai 2022.   Watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na watendaji wa ofisi ya Mkoa wa Ruvuma katika picha na Mgeni Rasmi, Mhe. Geophrey Pinda, leo tarehe 29 Julai 2022. Ruvuma XXXXXXXXXXXXXXXX   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amewataka Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria na Wasaidizi wao kutokiuka kanuni za Sheria ya Msaada wa Kisheria.   Mhe. Pinda ameyasema hayo leo tarehe 29 Julai, 2022 katika maadhimisho ya Tamasha la Majimaji ya Selebuka, linaloendelea kufanyika Wilayani Songea wakati akiongea na Watoa huduma ya Msaada wa Kisheria pamoja na Wasaidizi wa Kisheria.    “mnatakiwa kuwa nuru na washauri wema wa