NAIBU WAZIRI PINDA AKABIDHI VIFAA VYA KUENDESHEA MAHAKAMA MTANDAO


 XXXXXXXXXXX


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amekabidhi vifaa mbali mbali vya kuendeshea Mahakama mtandao  tarehe 18 Agosti, 2022 katika gereza la mahabusu Wilayani Mpanda. 

 

Vifaa hivyo ambavyo ni Kompyuta mpakato (Laptop) Luninga, Kamera na vingine, vitatumika kuendeshea Mahakama mtandao, ili kuweza kutatua kesi mbalimbali pamoja na kupunguza idadi kubwa ya mahabusu walioko katika gereza hilo.

 

Akiongea na maafisa wa gereza hilo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mhe. Pinda amesema dhamira ya Serikali ni kuondoa mlundikano wa mahabusu katika Magereza zetu.

 

Aidha, Mhe. Pinda amemuagiza DPP wa Mkoa wa Katavi ndugu Abel Mwandalama  kuondoa kesi zisizo na mashiko Ili kuondoa mlundikano wa mahabusu kwenye gereza hilo. 

 

Mhe. Pinda amemuagiza DPP kuhakisha kesi zinaendeshwa kwa weledi na kwa kuzingatia haki pamoja na kufanya upelelezi kwa wakati.

 

Mheshimiwa Pinda amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni tisa kwa ajili ya kujenga Mahakama shirikishi itakayojengwa hapa mpanda. Mahakama hiyo itajumuisha  Mahakama ya Mwanzo, Wilaya,  Mkoa,  Rufaa pamoja na Mahakama Kuu.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA