NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. GEOPHREY PINDA AWATAKA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA KUTOKIUKA KANUNI
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Geophrey Pinda akihutubia wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mkoa
wa Ruvuma, leo tarehe 29 Julai 2022.
. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Bibi. Mary Makondo akizungumza na watoa huduma ya msaada wa kisheria
kwa mkoa wa Ruvuma kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, leo tarehe 29 Julai 2022.
Watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja
na watendaji wa ofisi ya Mkoa wa Ruvuma katika picha na Mgeni Rasmi, Mhe.
Geophrey Pinda, leo tarehe 29 Julai 2022. Ruvuma
XXXXXXXXXXXXXXXX
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey
Pinda amewataka Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria na Wasaidizi wao kutokiuka
kanuni za Sheria ya Msaada wa Kisheria.
Mhe. Pinda ameyasema hayo leo tarehe 29 Julai,
2022 katika maadhimisho ya Tamasha la Majimaji ya Selebuka, linaloendelea
kufanyika Wilayani Songea wakati akiongea na Watoa huduma ya Msaada wa Kisheria
pamoja na Wasaidizi wa Kisheria.
“mnatakiwa kuwa nuru na washauri wema wa
kupinga dhuluma, unyanyasaji na vitendo vyote vya ukatili kupitia mifumo
mbalimbali iliyopo kuanzia ngazi ya kijiji/mtaa hadi Taifa” alisema Mhe. Pinda.
Aidha, Naibu Waziri amesema Wizara inatambua
mchango mkubwa unaofanywa na Watoa Huduma ya Msaada wa
Kisheria hapa nchini na itaendelea kuimarisha mashirikiano na wadau wote na
kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Bibi. Mary Makondo amewapongeza watoa huduma hao kwa kazi yao kwa
jamii, na kusisitiza wasivunjike moyo wanapokutana na changamoto bali iwe
chachu ya kufanya kazi zaidi katika kuwatumikia watanzania.
Comments
Post a Comment