WAZIRI NDUMBARO AZURU OFISI YA MASHTAKA NJOMBE


 XXXXXXXXXXXXXXXX


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro(Mb), ametembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Njombe akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu tarehe 18 Agosti 2022.

 

Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro amewaasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu.

 

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameainisha kuwa jitihada zinaendelea ili kuiwezesha Ofisi hiyo kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kwa kuona namna ya kuongeza bajeti kwa mwaka wa fedha ujao na kuendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali.

 

Dkt. Ndumbaro amekutana pia na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ambapo wamepata wasaa wa kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo haki jinai na utoaji haki kwa ujumla

 


Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA