WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA 400 MAJIMAJI SELEBUKA 2022, 81 WAKIPATIWA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA.
XXXXXXXXXXXXXXXXX
Wizara ya Katiba na Sheria imetoa huduma kwa wananchi zaidi
ya 400 katika Tamasha la Majimaji Selebuka lililomalizika leo 30 Julai, 2022
wilayani Songea-Ruvuma.
Akifunga Tamasha hilo Mbunge wa Songea Mjini ambaye pia ni
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza Wizara ya
Katiba na Sheria kwa kushiriki na kutoa huduma katika Tamasha hilo.
“Natoa pongezi kwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa ushiriki
wenu na huduma za msaada wa kisheria mliotoa kwa wananchi waliofika
kuwatembelea" alisema Dkt. Ndumbaro.
Katika tamasha hili lililoanza tarehe 23 Julai, Wizara kwa kushirikiana
na watoa huduma za msaada wa kisheria (paralegals) wametoa huduma za msaada wa
kisheria kwa wananchi 81 wilayani Songea.
Aidha, nakala 270 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na vipeperushi mbalimbali vya sheria ya ndoa, mtoto, mirathi na ardhi
vimegawiwa bure kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara.
Comments
Post a Comment