ZAIDI YA WANANCHI 200 WAPATA ELIMU YA MASUALA YA SHERIA KWENYE MAONESHO YA NANENANE MBEYA.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Mamia ya wahudhuriaji wamefurahishwa na Banda
la Wizara ya Katiba na Sheria kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye
Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Maonesho ya Nanenane Mwaka huu yamebeba kauli
mbiu isemayo; agenda 10/30 Kilimo ni biashara; jiandae kuhesabiwa kwa Mipango
bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye Banda
la Wizara ya Katiba na Sheria wamepata wasaa wa kujifunza na kuuliza maswali
mbalimbali hasa kuhusu sheria ya ndoa, ya ardhi, mirathi na sheria ya mtoto.
Zaidi ya wananchi 200 wamepatiwa elimu na
ushauri wa Kisheria.
Aidha, suala la mirathi ndio limekuwa
likiulizwa Kwa wingi na wananchi kupatiwa ufafanuzi na maelekezo ya kuweza
kutatua tatizo hilo.
Maonesho haya yamefungwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agosti, 08, 2022.
Comments
Post a Comment