RAIS SAMIA ATAKA SHERIA YA KULINDA UWEKEZAJI IANGALIWE UPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akizindua Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Mfumo wa Usajili wa Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Dodoma. Sehemu ya Mawakili wa Serikali wakimsikiliza Rais. XXXXXXXXXXXXXXXXXX Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia upya sheria ya Uwekezaji nchini ili kuepuka migongano na migogoro kati ya nchi na Wawekezaji. Rais Samia ameyasema hayo wakati akizindua Chama cha Mawakili wa Serikali katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre leo tarehe 29 Septemba, 2022, amba...