BUNGE LIMERIDHIA ITIFAKI YA KUIONGEZEA MAMLAKA MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha hoja ya kuliomba Bunge kuridhia itifaki ya kuiongezea mamlaka Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

XXXXXXXXXXXX

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia itifaki ya kuiongezea mamlaka  Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hoja ya kuomba kuridhiwa kwa Itifaki hiyo limewasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo, Septemba 20, 2022 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika wasilisho hilo Dkt. Ndumbaro amesema kuridhiwa kwa Itifaki hiyo kutawezesha nchi wanachama kuwa na Umoja wa Forodha, Soko Huria, Sarafu ya Pamoja na kuwezesha wananchi kuwa na haki ya kuishi kwenye nchi yoyote kati ya nchi wananchama bila bughudha ili mradi uwe na shughuli halali.

Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akichangia hoja wakati wa wasilisho hilo amesema itifaki hii itatufaa sana nchi na wananchi wa Tanzania kwani itawezesha wananchi hususan wafanyabiashara kuingia ndani ya nchi nyingine na kuvumbua fursa mbalimbali za kiuchumi.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria waliochangia mjadala wakati wa wasilisho hilo wamesema nchi ikiridhia Itifaki hiyo wananchi watakuwa na uhuru wa kuingia, kufanya kazi na kupata huduma kwa nchi wanachama pia kutawezesha kutatua migogoro ya kibiashara.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA