NAIBU WAZIRI PINDA AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akizungumza na Menejimenti ya RITA.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatib kazungu akizungumza na Menejimenti ya RITA.
Picha ya pamoja.
Naibu waziri Mhe. Geophrey Mizengo Pinda
amewataka watumishi kuheshimu na kuzingatia Sheria za utumishi wa Umma sambamba
na kuheshimiana kila mmoja wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
# Ameyasema hayo leo tarehe 6 Septemba, 2022
Jijini Arusha wakati akizungumza na Menejimenti ya RITA katika kikao kazi Cha
kuwajengea uelewa katika kuzingatia kanuni, miongozo ya utumishi wa Umma ili
Kuunga mkono jitihada za Serikali za kiwaletea Maendeleo wananchi.
#Mhe. Pinda ameongeza kuwa Menejimenti
inatakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi na kufuata misingi ya Sheria,
uadilifu na busara hasa itakapotokea mtumishi amekwenda kinyume na kutakiwa
kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
# Pia ameagiza kila kiongozi kukubali
mabadiliko ya uongozi kuanzia ngazi ya Serikali kuu, Wizara na ndani ya Taasisi
ili kwa pamoja Kuunga mmono na kutekeleza maelekezo ya Serikali iliyopo
madarakani kwa Sasa.
#Kuhusu uvujishaji wa Siri ya vikao vya ndani
wakati wa kufanya maamuzi Mhe. Pinda amesema katika utendaji wa Serikali tabia
hiyo ni sumu mbaya na haikubaliki kwani inasababisha migogoro na kushindwa
kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa wakati kwa baadhi ya watumishi
wasiyotekeleza majukumu yao ipasavyo.
#Mhe. Pinda amesisitiza mnyororo wa
Mawasiliano baina ya Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria kwani
ndiyo chombo pekee cha kuzitetea na kuziwakilisha katika vikao vya juu
vya maamuzi ikiwemo makadirio ya bajeti ya Wizara na Taasisi zake.
" Wizara tunawajibika kwa Serikali kutoa
taarifa ya utekelezaji wa kila Taasisi iliyopo chini ya Wizara hii hivyo
ni muhimu Menejimenti zote kutambua wajibu wenu Kwetu kama viongozi wenu wa
kuwasemea katika vikao vya maamuzi vya Kitaifa".Alisema Mhe.Pinda.
# Mhe. Pinda amewapongeza Wafanyakazi na
Menejimenti ya RITA kwa kushirikiana vizuri na Wizara katika utekelezaji wa
mikakati mbalimbali ikiwemo ya Usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano
katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo watoto zaidi ya 7.5 wamesajiliwa na
kupatiwa vyeti vya Kuzaliwa bila ya malipo.
# Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary
Makondo amesema Wizara inapokea na kufanyia kazi mahitaji ya kila Taasisi hivyo
RITA isisite kuwasilisha mahitaji kwa wakati.
# Kwa upande wake Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa
Mtendaji Mkuu wa RITA Bi. Angela Anatory amesema kikao hicho kinafanyika wakati
muafaka kutokana na mabadiliko ya uongozi yaliyofanyika ili kwa pamoja
kushirikiana kuboresha na kubuni upya mikakati itakayosaidia kufikia malengo ya
kutoa huduma bora kwa Wananchi.
# Aidha ameishukuru Wizara kwa kukubali
kufanyika Kwa kikao kazi hicho hivyo kuahidi kupokea na kutekeleza maelekezo na
ushauri wa viongozi Wakuu wa Kitaifa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
"Mhe. Naibu Waziri tunakuahidi kama
Menejimenti tutashirikiana na Wizara yako kuhakikisha tunatekeleza maagizo yote
na tutawajibika ipasavyo ili RITA isonge mbele". Alisema Bi. Anatory.
# Kikao kati ya Wizara ya Katiba na Sheria na
Menejimenti ya RITA kitaendelea Kwa siku tatu na kutatolewa mafunzo maalum ya
uongozi, Sheria na miongozo ya utumishi wa Umma.
Comments
Post a Comment