NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE GEOPHREY MIZENGO PINDA(MB) AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA SHIRIKA LA MASHAURIANO YA SHERIA ZA KIMATAIFA JIJINI NEW DELHI NCHINI INDIA


 



XXXXXXXXXXXXXXXXXX

Leo tarehe 26.09.2022 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Mizengo Pinda ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 60 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria za Kimataifa la Nchi za Asia  na Afrika (AALCO) uliofanyika Jijini New Delhi nchini India.

Katika Mkutano huu Mhe. Naibu Waziri amewasilisha salamu za shukrani kama Rais wa 59 wa Shirikisho hilo  anayemaliza muda wake.

Mkutano huu unaofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Septemba 2022, masuala mbalimbali yanatarajiwa kujadiliwa ikiwemo Mabadiliko ya Tabia Nchi, Biashara na uwekezaji, Mazingira na Ugaidi, Masuala ya Wakimbizi na Tume ya kimataifa inayoshughulikia maendeleo ya Sheria za Kimataifa 

Katika Mkutano huu Mhe. Naibu Waziri ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini India, Bi Hanisa Mbega, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt  Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria Bwana Griffin Mwakapeje na Ofisa wa Wizara wa Mambo ya Nje Kitengo cha Sheria Bwana Paul Makelele.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA