WABUNGE WAPATIWA SEMINA KUHUSU MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA



                                        Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akichangia mada.


                                        Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda akichangia mada.

 
Wabunge wakisikiliza mada 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yapatiwa semina kuhusu marekebisho ya sheria ya ndoa ya Mwaka 1971.

Semina hiyo kwa Wabunge imetolewa na Wataalam wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 21 Septemba, 2022.

Katika semina hiyo Serikali imesema imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka makundi mbalimbali ya wananchi Ili kuona namna bora ya kufanyia marekebisho sheria hiyo.

Katika mjadala wa semina hiyo jambo kubwa lililojitokeza ni umri sahihi wa mtu kuoa au kuolewa na namna umri  unavyotafsiriwa katika suala hilo Kwa upande wa dini.

Dkt. Ndumbaro amesema katika sheria ya ndoa sio kila kitu hakifai, vipo ambavyo vitaendelea kuwepo.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walishauri marekebisho ya sheria hiyo yazingatie wakati na mazingira tuliyopo sasa ili itakapokamilika  itumike bila kuleta migongano.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Najma Giga alisisitiza kuwa Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la talaka hivyo marekebisho ya sheria hiyo yaangalie chanzo cha talaka na namna ya kuzipunguza au kuziondoa kabisa katika jamii.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA