WAZIRI NDUMBARO AZINDUA KAMPENI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA


 


XXXXXXXXXXXXXXX


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amezindua  kampeni ya utoaji wa huduma za  msaada wa Kisheria tarehe 8 Septemba 2022, Jijini Arusha.

 

 Wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Ikiding'a, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Dkt. Ndumbaro amesema Utoaji wa hudumu za msaada wa kisheria utamsaidia mwananchi mnyonge kupata huduma za Mawakili pasipo na malipo.

 

 "Serikali inatambua kuwa siyo kila mwanachi ana uwezo wa kulipia gharama za kisheria, hivyo katika huduma hii tuna wadau mbali mbali ambao tunashirikiana nao  kama vile TLS, TAWLA, Asasi za kiraia, pamoja na wadau wengine". alisema Dkt. Ndumbaro

 

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameshiriki pia kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa  kuhudumia wananchi mbali mbali kama Wakili.

 

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA