Posts

Showing posts from October, 2022

MAELEKEZO YA RAIS SAMIA YAANZA KUTEKELEZWA NA WIZARA

Image
  XXXXXXXXXXXX Wataalam wa Wizara ya Katiba na Sheria waanza kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupitia sheria za usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji. Maagizo hayo yalitolewa na Rais Samia katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika mwishoni mwa mwezi Septemba, 2022 jijini Dodoma. Rais Samia alitoa maagizo hayo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wawekezaji namna migogoro ya uwekezaji inapotokea na inavyosuluhishwa na kuonekana kupendelea upande mmoja.

KUTUNGWA KWA SHERIA YA UFILISI KUTAPUNGUZA CHANGAMOTO ZA MFUMO WA UFILISI NCHINI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Dkt. Joseph Mhagama akiongea wakati wa u wasilishaji wa taarifa ya RITA kuhusu mafanikio na changamoto katika utekelezaji    wa uratibu wa majukumu ya usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu, Ufilisi na Udhamini Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi. Angela Anatory akiwasilisha taarifa kuhusu mafanikio na changamoto katika utekelezaji  wa uratibu wa majukumu ya usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu, Ufilisi na Udhamini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria XXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Taasisi nyingi zimekuwa zinafanya ufilisi nchini kutokana na kuwa na sheria nyingi za ufilisi, hivyo kukiwa na sheria ya ufilisi moja kutawezesha Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) waendelee na shughuli yake ya ufilisi kwani ndiyo Taasisi pekee iliyopewa jukumu la ufi

DKT NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI TANZANIA NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA WATOTO NCHINI (UNICEF)

Image
                                                         XXXXXXXXXXX Mhe. Dkt Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Ndg. Zlatan Milisic na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Watoto nchini (UNICEF) Jijini Dodoma leo tarehe 26 Oktoba, 2022.   Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo ushirikiano baina ya Mashirika hayo na Wizara katika masuala ya Haki za Binadamu ikiwemo haki za Watoto, Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na mchakato unaoendelea kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ndoa.  

DKT. KAZUNGU AAHIDI USHIRIKIANO NA WADAU KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WATOTO

Image
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazunguakisoma hotuba yake wakati  akifunga kikao kazi cha Haki Mtoto cha siku mbili cha Wadau wa Jukwaa la Haki Mtoto kilichofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 21 Oktoba, 2022 jijini Arusha Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Felistas Mushi akimkaribisha mgeni rasmi kufunga  kikao kazi cha Haki Mtoto cha siku mbili cha Wadau wa Jukwaa la Haki Mtoto kilichofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 21 Oktoba, 2022 jijini Arusha. Washiriki wa kikao kazi wakimsikiliza mgeni rasmi. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXX Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu ameahidi Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kushirikiana na Wadau ili kushughulikia ulinzi na haki ya mtoto. Dkt. Kazungu ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha Haki Mtoto cha siku mbili cha Wadau wa Jukwaa la Haki Mtoto kilichofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 21 Oktoba, 2022 jijini Arusha. Dkt

KIKAO CHA 73 CHA KAMISHENI YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geophrey Mizengo Pinda  akiwa katika kikao cha 73 Cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (The Ordinary Session of the African Commission on Human & People's Rights) kinachofanyika Banjul, Gambia kuanzia Oktoba 21 hadi Novemba 9, 2022. Washiriki wa kikao.

RAIS SAMIA ASISITIZA ELIMU YA SHERIA KWA WANANCHI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiongea katika    maadhimisho ya miaka 25 ya kuwepo kwa Taasisi ya WiLDAF tarehe 20 Oktoba, 2022 Jijini Dar es Salaam.                                                                                                                                                                      Meza kuu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimkaribisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuongea na wanannchi katika   maadhimisho ya miaka 25 ya kuwepo kwa Taasisi ya WiLDAF tarehe 20 Oktoba, 2022 Jijini Dar es Salaam.                                                                                                                                        Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Shertia Bi. Mary Makondo (wa tatu kulia) na waalikwa wengine wakimsikiliza Rais.  XXXXXXXXXXXXXX Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesisitiza elimu ya sheria kuendelea kutole

WADAU WA HAKI MTOTO WATAKIWA KUTOA TAARIFA NA TAKWIMU SAHIHI KUHUSU UKATILI DHIDI YA WATOTO

Image
Mkurugenzi wa Kitengo cha Msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Felistas Mushi akiongea na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kikao cha siku mbili cha Jukwaa la Haki Mtoto kinachofanyika Oktoba 20 na 21,  jijini Arusha. Washiriki wa kikao cha siku mbili cha Jukwaa la Haki Mtoto kinachofanyika Oktoba 20 na 21,  jijini Arusha. Mwakilishi kutoka UNICEF Bi. Victoria Mgonela akiongea na washiriki wa  kikao cha siku mbili cha Jukwaa la Haki Mtoto kinachofanyika Oktoba 20 na 21,  jijini Arusha. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXX Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amewataka wadau wa Haki Mtoto kujikita katika majukumu yao na kutoa taarifa na takwimu sahihi  dhidi ya ukatili wa watoto ili kuwezesha Serikali inapopanga afua iwe na taarifa na takwimu sahihi zitakazowezesha kupanga mikakati ambayo itasaidia kutokomeza au kupunguza vitendo hivyo vya ukatili. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheri

MSAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA AWATAKA WATOA HUDUMA HIZO WAJISAJILI KWENYE MFUMO

Image
Mwakilishi wa Msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Agness Mkawe a kiongea kwenye  warsha iliyoandaliwa na Shirika la Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility) leo tarehe 19 Oktoba, 2022. Washiriki wa Warsha wakimsikiliza mgeni rasmi. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXX Msajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria amewataka watoa huduma za msaada wa kisheria kujisajili kwenye mfumo wa usajili wa kutoa huduma za msaada wa kisheria  Akiongea kwenye  warsha iliyoandaliwa na Shirika la Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility) leo tarehe 19 Oktoba, 2022 mwakilishi wa Msajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria  Bi. Agness Mkawe amesema " Wizara inataka watoa huduma wote za msaada wa kisheria nchini kujisajili kwenye mfumo  wa usajili wa watoa huduma ya msaada wa kisheria ambao ni   www.legalaid.go.tz Bi. Mkawe amesema Serikali  ilisha ondoa ada ya usajili ambayo ilikuwa ni shilingi 30,000

TAARIFA KWA UMMA

Image
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA   Telegramu:   ‘‘LEGAL’’ Simu Na.:     +255 26 2310019 Nukushi:      +255 26 2310056 Barua Pepe:km@sheria.go.tz Tovuti:   www.sheria.go.tz               Mji wa Serikali Mtumba,              Mtaa wa Katiba,                S. L. P. 315,                40484 DODOMA.       T A N G A Z O   K W A   U M M A Kufuatia taarifa ya matokeo ya wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo ya hivi karibuni, na baada ya kuibuka kwa taharuki miongoni mwa wanajamii wakiwemo wanazuoni na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria kuhusu ufaulu mdogo wa wanafunzi   katika tasnia ya Sheria, tarehe 12 Oktoba, 2022 Mheshimiwa Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria aliunda Kamati Maalum ya kufanya tathmini ya mfumo wa elimu ya Sheria nchini na changamoto zinazoukabili

WIZARA YA KATIBA KUTOA HUDUMA ZA KISHERIA KIDIJITALI – DKT NDUMBARO

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akifungua warsha ya siku mbili kwa watoa Huduma za Msaada wa Kisheria. Washiriki wakiendelea na pamoja. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wizara ya Katiba na Sheria imekusudia kuhakikisha huduma za kisheria zinazotolewa na Wizara na Taasisi zilizo chini yake zinapatikana kwa njia ya TEHAMA. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria, Wasaidizi wa Kisheria, Mawakili, Wanasheria na Maafisa wa Jeshi la Magereza ambayo inafanyika kuanzia leo Oktoba 17, 2022 Jijini Arusha. Dkt Ndumbaro amesema “Kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA kwenye utoaji wa huduma, Wizara ya Katiba na Sheria imekusudia kuhakikisha huduma za kisheria zinazotolewa na Wizara na Taasisi zilizo chini yake zinapatikana kwa njia ya TEHAMA. Hili litawezesha huduma kupatikana kwa wakati na hatimaye kuwezesha vyombo vingine vya utoaji haki kuto

NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA MIKATABA IANDIKWE KWA KISWAHILI

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akizungumza kabla ya kupokea Taarifa za Tathmini za Utekelezaji wa Sheria mbalimbali. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) akipokea Taarifa za Tathmini za Utekelezaji wa Sheria mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu Mhe. January Msofe.   Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amesema mikataba yote iandikwe kwa Kiswahili ili kuwezesha kueleweka kiurahisi kwa wanaohusika na mikataba hiyo. Naibu Waziri Pinda ameyasema hayo leo Oktoba13, 2022 wakati akipokea taarifa nane za tathmini za utekelezaji wa sheria mbalimbali nchini. Naibu Waziri Pinda amesema "tuhakikishe Kiswahili kinaheshimika katika mikataba ili kuwezesha wanaoingia mikataba hiyo kuelewa vizuri kilichomo ili kuepuka matatizo mbalimbali" Mhe. Pinda alisisitiza "hili ni eneo muhimu sana katika maendeleo ya Taifa letu na ndio maana sheria zote zina

DKT. MWAKYEMBE KUONGOZA KAMATI YA WATU SABA KUCHUNGUZA MATOKEO LAW SCHOOL

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na waandishi wa habari. XXXXXXXXXXXXXXXX Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeunda Kamati ya watu saba kuchunguza na kushughulikia malalamiko ya matokeo ya wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati akiongea na Vyombo vya Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Jijini Dodoma  tarehe 12 Oktoba, 2022. Dkt. Ndumbaro amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaposikia malalamiko inachukua hatua na hivyo imeamua kuunda kamati itakayotoa majibu ya malalamiko ya wanafunzi wa Chuo hicho. Dkt. Ndumbaro amesema "Sisi kama Serikali ya Awamu ya Sita tunaposikia malalamiko tunachukua hatua, ili kama kuna tatizo lazima tulijue." Dkt. Ndumbaro aliongeza "Serikali imeamua kuunda Kamati ya watu saba ambayo imepewa siku 30 kuanzia Oktoba 13, 2022 ili kutuambia tatizo liko wapi." Dkt. Ndumbaro

WAZIRI NDUMBARO ATEMBELEA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA KESI ZA MASALIA YA MAUAJI YA KIMBARI

Image
            XXXXXXXXXXXXXX Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria akiongozana na viongozi wengine wa Wizara wametembelea Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari – IRMCT Jijini Arusha tarehe 10 Oktoba, 2022 na kufanya mazungumzo na Msajili wa Mahakama hiyo Jaji Abubacarr Tambadou. Mazungumzo hayo yalihusu uendeshaji wa Mahakama hiyo na mahusiano yake na Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na amani na utulivu duniani.  Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Ndumbaro aliongozana na Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu na Wataalam kutoka Wizarani.

KIKAO CHA WADAU KAMATI YA TATHMINI YA MRADI WA ACCESS TO JUSTICE AND RULE OF LAW

Image
 XXXXXXXXXXXXXX Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo ameshiriki kikao cha Wadau Kamati ya Tathmini ya Mradi wa Access to Justice and Rule of Law (Local Project Appraisal Comittee) unaofadhiliwa na UNDP. Kikao hicho kilifanyika tarehe 4 Oktoba, 2022 Jijini Dar es Salaam.    Kikao kilipitia andiko la mradi na kutoa mapendekezo ya kuanza utekelezaji wake. Mradi huo ni wa miaka mitatu 2022/23 - 2024/25, na ni mwendelezo wa mradi wa Access to Justice and Human Rights Protection ulioisha mwaka 2021.    Mradi utatekelezwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka - NPS, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - CHRAGG, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Magereza na Polisi.  

IDARA NA SEKTA ZINAZOHUSIKA NA UTAJIRI ASILI NA MALIASILIA ZIFANYE KAZI KWA PAMOJA: BI. MAKONDO

Image
  XXXXXXXXXXXXXXXXX Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amezitaka Idara na Sekta za Serikali zinazohusika na usimamizi wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wananchi wananufaika na utajiri asilia na maliasilia za nchi.    Bi. Makondo ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Mpango wa Kusimamia Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi (Natural Wealth and Resources Socio-Economic Governance Programme) leo tarehe 6 Oktoba, 2022 Jijini Arusha.   “Najua mnawakilisha ofisi zenu, mnawakilisha Wizara zenu lakini tukumbuke tu wamoja, tunajenga Tanzania moja hivyo tufanye kazi kwa pamoja kuhakikisha mpango huu haupunguzi tu  umaskini kwa Watanzania bali pia unaongeza Pato la Taifa.” Alisema Bi Makondo.   Mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa ufadhili wa Serikali na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).   Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo y