DKT NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI TANZANIA NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA WATOTO NCHINI (UNICEF)

XXXXXXXXXXX
Mhe. Dkt Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria amekutana na kufanya
mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Ndg. Zlatan
Milisic na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia
Watoto nchini (UNICEF) Jijini Dodoma leo tarehe 26 Oktoba, 2022.
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo
ushirikiano baina ya Mashirika hayo na Wizara katika masuala ya Haki za
Binadamu ikiwemo haki za Watoto, Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na
mchakato unaoendelea kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ndoa.
Comments
Post a Comment