KIKAO CHA WADAU KAMATI YA TATHMINI YA MRADI WA ACCESS TO JUSTICE AND RULE OF LAW


 XXXXXXXXXXXXXX

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo ameshiriki kikao cha Wadau Kamati ya Tathmini ya Mradi wa Access to Justice and Rule of Law (Local Project Appraisal Comittee) unaofadhiliwa na UNDP. Kikao hicho kilifanyika tarehe 4 Oktoba, 2022 Jijini Dar es Salaam. 

 

Kikao kilipitia andiko la mradi na kutoa mapendekezo ya kuanza utekelezaji wake. Mradi huo ni wa miaka mitatu 2022/23 - 2024/25, na ni mwendelezo wa mradi wa Access to Justice and Human Rights Protection ulioisha mwaka 2021. 

 

Mradi utatekelezwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka - NPS, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - CHRAGG, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Magereza na Polisi.

 


Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA