MSAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA AWATAKA WATOA HUDUMA HIZO WAJISAJILI KWENYE MFUMO


Mwakilishi wa Msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Agness Mkawe akiongea kwenye  warsha iliyoandaliwa na Shirika la Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility) leo tarehe 19 Oktoba, 2022.


Washiriki wa Warsha wakimsikiliza mgeni rasmi.


Picha ya pamoja.

XXXXXXXXXXXXXX

Msajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria amewataka watoa huduma za msaada wa kisheria kujisajili kwenye mfumo wa usajili wa kutoa huduma za msaada wa kisheria 

Akiongea kwenye  warsha iliyoandaliwa na Shirika la Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility) leo tarehe 19 Oktoba, 2022 mwakilishi wa Msajili wa watoa huduma za msaada wa kisheria  Bi. Agness Mkawe amesema " Wizara inataka watoa huduma wote za msaada wa kisheria nchini kujisajili kwenye mfumo  wa usajili wa watoa huduma ya msaada wa kisheria ambao ni  www.legalaid.go.tz

Bi. Mkawe amesema Serikali  ilisha ondoa ada ya usajili ambayo ilikuwa ni shilingi 30,000 na kufanya usajili kuwa bure lakini mpaka sasa bado watoa huduma wengine hawajajisajili kitu ambacho ni kosa la kisheria, hivyo wote tunatakiwa kujisajili. 

Akitoa takwimu za mashirika yaliyojisajili  Bi. Mkawe amesema "mpaka sasa ni mashirika 220 pamoja na wasaidizi wa kisheria 1047 ambao  tayari wamejisajili kwenye mfumo wa usajili wa watoa huduma ya msaada  wa kisheria "

Aidha, amewapongeza wote wanaotoa huduma za msaada wa kisheria  na kusema " Wizara inatambua mchango wenu mkubwa mnaofanya katika kusaidia na kutatua kesi mbali mbali za wananchi wakati wa kutoa huduma ya msaada wa kisheria hongereni sana" 

Naye Meneja wa programu kutoka Shirika la Mfuko wa Huduma za Kisheria( Legal Services Facility ) Bw. Deogratias Bwire ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa ushiriakiano wanaowapa pale wanapokwama   wakati wa kutoa huduma ya msaada wa kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA