NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA MIKATABA IANDIKWE KWA KISWAHILI

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akizungumza kabla ya kupokea Taarifa za Tathmini za Utekelezaji wa Sheria mbalimbali.



Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) akipokea Taarifa za Tathmini za Utekelezaji wa Sheria mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu Mhe. January Msofe.



 

Picha ya pamoja.

XXXXXXXXXXXXXXXX

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amesema mikataba yote iandikwe kwa Kiswahili ili kuwezesha kueleweka kiurahisi kwa wanaohusika na mikataba hiyo.

Naibu Waziri Pinda ameyasema hayo leo Oktoba13, 2022 wakati akipokea taarifa nane za tathmini za utekelezaji wa sheria mbalimbali nchini.

Naibu Waziri Pinda amesema "tuhakikishe Kiswahili kinaheshimika katika mikataba ili kuwezesha wanaoingia mikataba hiyo kuelewa vizuri kilichomo ili kuepuka matatizo mbalimbali"

Mhe. Pinda alisisitiza "hili ni eneo muhimu sana katika maendeleo ya Taifa letu na ndio maana sheria zote zinarudishwa katika lugha ya Kiswahili ili watu waweze kuzielewa kirahisi".

Aidha, Mhe. Pinda amesema Wizara imepokea taarifa hizo na itahakikisha zinawafikia walengwa na kufuatilia utekelezwaji wake.

Awali akiwasilisha taarifa hizo Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe. Jaji Mstaafu January Msofe amesema Tume hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake imeweza kuwasilisha taarifa nane kwa mara moja ambapo miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji zinazosimamia Sekta ya Mifugo na Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria zinazosimamia Adhabu Mbadala.

 


Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA