TAARIFA KWA UMMA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Telegramu: ‘‘LEGAL’’ Simu Na.: +255 26 2310019 Nukushi: +255 26 2310056 Barua Pepe:km@sheria.go.tz Tovuti: www.sheria.go.tz |
|
Mji wa Serikali Mtumba, Mtaa wa Katiba, S. L. P. 315, 40484 DODOMA. |
T A N G A Z
O K W A U M M A
Kufuatia
taarifa ya matokeo ya wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
ya hivi karibuni, na baada ya kuibuka kwa taharuki miongoni mwa wanajamii
wakiwemo wanazuoni na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria kuhusu ufaulu mdogo
wa wanafunzi katika tasnia ya Sheria,
tarehe 12 Oktoba, 2022 Mheshimiwa Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb.), Waziri wa
Katiba na Sheria aliunda Kamati Maalum ya kufanya tathmini ya mfumo wa elimu ya
Sheria nchini na changamoto zinazoukabili mfumo huo ikiwa ni pamoja na namna mafunzo
ya uanasheria kwa vitendo yanavyotolewa.
Pamoja
na mambo mengine, Kamati hiyo imepewa jukumu la kushauri namna ya kuboresha
mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya taaluma ya Sheria kwa lengo la kuwa na
ushindani wa kitaifa na kimataifa. Kamati katika utekelezaji wa majukumu yake
kwa mujibu wa Hadidu za Rejea ilizopewa, itapokea maoni kwa maandishi pia
kuwasikiliza wadau mbalimbali ana kwa ana.
Kwa
kuwa siyo wananchi wote watapata fursa ya kufika mbele ya Kamati kutoa maoni, Mhe.
Dkt. Harrison G. Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati anawaalika wananchi na wadau
wenye mapenzi mema na uboreshaji wa mfumo wa elimu ya sheria nchini na elimu ya
uanasheria kwa vitendo, kuwasilisha maoni kwa maandishi ili kuiwezesha Kamati kupata
maoni mengi kadri inavyowezekana na hatimaye kushauri ipasavyo. Mwisho wa
kupokea maoni ya maandishi ni tarehe 24 Oktoba, 2022 saa 10:00 jioni.
Maoni
hayo yawasilishwe kupitia barua pepe ya km@sheria.go.tz,
mitandao ya kijamii ya twitter: @Sheria_Katiba; Instagram @katibanasheria_ au WhatsApp
kwa namba 0742 910529.
IMETOLEWA
NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
18 Oktoba, 2022
Comments
Post a Comment