WAZIRI NDUMBARO ATEMBELEA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA KESI ZA MASALIA YA MAUAJI YA KIMBARI


 
        

XXXXXXXXXXXXXX

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria akiongozana na viongozi wengine wa Wizara wametembelea Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari – IRMCT Jijini Arusha tarehe 10 Oktoba, 2022 na kufanya mazungumzo na Msajili wa Mahakama hiyo Jaji Abubacarr Tambadou.

Mazungumzo hayo yalihusu uendeshaji wa Mahakama hiyo na mahusiano yake na Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na amani na utulivu duniani. 

Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Ndumbaro aliongozana na Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu na Wataalam kutoka Wizarani.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA