Posts

Showing posts from November, 2022

WAZIRI NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA KITUO JUMUISHI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022.  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Khatibu Kazungu akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022.  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza leo Novemba 29, 2022.  Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Patience Ntwina. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro amepongeza jitihada hizo na ushirikiano uliooneshwa kat

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KUANDAA MPANGO KAZI WA UFUATILIAJI NA TATHIMINI.

Image
 XXXXXXXXXXX Wizara ya Katiba na Sheria inaandaa Mpango Kazi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa mwaka wa shughuli zote za Wizara.  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera, Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini ndugu Emmanuel Mayeji kwenye kikao kazi cha siku tano kinachofanyika kuanzia tarehe 28 Novemba hadi 2 Desemba 2022 mjini Morogoro.  Ndugu Mayeji  amesema " kakao hiki  kina malengo makuu mawili , Moja  kujadili namna ya kuwa na mfumo thabiti wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni , Miongozo na Mipango inayosimamiwa" Mbili kuwa na mfumo  thabiti wa utoaji wa taarifa  za utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kuzingatia takwimu sahihi za mafanikio na changamoto zilizojitokeza pamoja na kuwa na  mkakati wa kutatua changamoto zilizojitikeza wakati wa utekelezaji" . Aidha kikao kazi hicho kinahudhuriwa na  maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

JIUNGENI NA CHAMA CHA MAWAKILI CHA AFRIKA MASHARIKI- MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Image
  XXXXXXXXXXXXX Rais Samia Suluhu Hassan  amewataka Mawakili  nchini kujiunga na Chama Cha Mawakili Cha Afrika Mashariki (East Africa Law Society). Mheshimiwa Rais ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa  Chama Cha Mawakili Cha Afrika Mashariki tarehe 24 Novemba, 2022 Jijini Arusha . Akiongea kwenye kikao hicho Mhe. Rais amesema "Afrika Mashariki Sasa ni wamoja tunafanya kazi kwa kushirikiana, na nyinyi shirikianeni kutatua kesi mbalimbali ndani ya Jumuiya yetu na nje ya Jumuiya, kuweni wamoja na imara  katika kujenga Chama chenu"  Aidha Mheshimiwa Rais amewaomba Mawakili  kuwakaribisha Mawakili kutoka DRC Congo , ambao wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi karibuni.  Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda  ambaye alimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  amesema " ni fursa kwa Mawakili   wetu kufanya kazi ndani ya Afrika Mashariki kwasababu watajijengea  uwezo na kujifunza mambo mengi kutoka kw

KIKAO KAZI

Image
  XXXXXXXXXXXXX Wataalam kutoka Wizara ya Katiba na sheria na Taasisi zilizo chini yake wakutana mjini Morogoro kwa kikao kazi cha siku tano kuanzia Novemba 22 hadi 26, 2022 kuandaa vipaumbele vya Wizara kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024. Pia katika kikao hicho watajadiliana  kuhusu maandalizi ya kuanza Kwa awamu ya pili ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Mtaalam Mwelekezi alipofanya utafiti juu ya changamoto zinazoikabili sekta ya sheria.

DKT. NDUMBARO ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

Image
 XXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro anashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Balaclava, nchini Mauritius kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba, 2022. Mkutano huo umefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Pravind Kumar Jugnauth. Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali katika sekta ya sheria yakiwemo masuala ya upatikanaji haki, Haki za Binadamu, matumizi ya akili bandia katika mifumo ya Mahakama, umuhimu wa sekta ya sheria katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Mambo mengine yanayotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Urejeshwaji wa Wahalifu, Mikataba ya Uwekezaji, Hatua zilizochokuliwa na Nchi Wanachama katika maeneo mbalimbali yakiwemo Mapambano dhidi ya Rushwa, Sheria za Kudhibiti uhalifu wa mtandao, Ushirikiano katika masuala ya Jinai na Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala na  wajibu wa Vyombo vya Habari katika kutekeleza Haki ya Kutoa Maoni. Mkuta

MALALAMIKO YA WANAFUNZI WA LAW SCHOOL HAYANA USHAHIDI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akipokea ripoti ya tathmini ya mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (law school) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo. Dkt. Ndumbaro akikabidhi ripoti kwa Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo. Dkt. Ndumbaro akikabidhi ripoti kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu. Mwenyekiti wa Kamati Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia) akielezea jambo. Picha ya Viongozi wa wizara na Wajumbe wa Kamati. XXXXXXXXXXXXXXXX Kamati ya Tathmini ya Mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Kwa Vitendo Tanzania yakosa ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za rushwa, uonevu na upendeleo katika utungaji na usahihishaji wa mitihani zilizotolewa na wanafunzi wa kundi la 33. Hayo yamebainishwa Leo Novemba 20, 2022 wakati Kamati hiyo ikikabidhi ripoti ya tathmini hiyo Kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbar

JUKUMU LA KUHIFADHI WAKIMBIZI SIYO JEPESI HASA KWA NCHI WENYEJI- MHE PINDA

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey  Pinda   akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kujadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi na Wahamiaji kilichofanyika jijini, Arusha. Washiriki wa kikao. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey  Pinda amesema  kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na  changamoto  ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokimbia makazi yao  jukumu la kuhifadhi Wakimbizi ni jukumu zito hasa kwa nchi inayopokea Wakimbizi.  Mhe. Pinda ameyasema hayo  wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kujadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi na Wahamiaji kilichofanyika  kuanzia tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 jijini Arusha. Katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema " Serikali imekuwa ikihifadhi Wakimbizi kwa muda mrefu, hivyo inatambua mchango mkubwa wa wadau wa masuala ya Wakimbizi katika nyanja zote". Aidha, Mhe. Pinda amesema "kama mnavyofahamu  Wakimbizi wengi  wanahifadhiwa katika nchi zinazoendelea na Tanzania tu

DKT. NDUMBARO AIASA JAMII KUACHA VITENDO VYA UKATILI

Image
Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya akifungua kikao cha mtandao wa masuala ya familia kuhusu upatikanaji wa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia. Meza kuu. Washiriki. Picha ya pamoja.  XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiasa jamii kuachana na Vitendo vya ukatili wa kijinsia. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya kwa niaba ya Dkt. Ndumbaro katika ufunguzi wa kikao cha mtandao wa masuala ya familia na Wadau kutoka  Wizara  mbalimbali kuhusu upatikanaji wa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika Novemba 16, 2022 mjini Morogoro. Amesema, "kama tunataka kuwa na jamii imara, ni lazima sote tuungane na kupinga Vitendo vyovyote vya ukatili" Vilevile, katika hotuba yake Dkt. Ndumbaro amewataka Wadau hao kusaidiana na serikali kutoa elimu na kuendelea kukemea vitendo vya ukatili kwani hata kama

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA IMEJIPANGA KUBORESHA MIUNDOMBIMU YA MAHAKAMA

Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same.     XXXXXXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey Mizengo Pinda amesema  Wizara imejipanga kuhakikisha miundombinu ya Mahakama inakuwa bora. Mhe. Pinda amesema hayo jana tarehe 15 Novemba, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Pinda amesema "Serikali  yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan   inahakikisha mazingira ya utoaji haki katika Mahakama zetu yanakuwa bora na rafiki, na tayari kwa mwaka huu tunashuhudia Mahakama mbalimbali zikijemgwa,  tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais." Aidha, Jaji Mkuu Mheshimiwa Prof. Ibrahimu Juma amesema Mahakama imejiwekea mkakati kuhakikisha  inaendelea kujenga majengo ya Mahakama kwa zile Wilaya ambazo majengo yao yamechakaa ili kuhakikisha wanasogeza  huduma ya haki kwa Wananchi. Ak

TAASISI ZA HAKI JINAI ZAANDAA MFUMO WA KUBADILISHANA TAARIFA

Image
Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Ernest Mbuna akitoa mada katika kikao cha maandalizi ya mfumo wa Haki Jinai. Washiriki wa kikao kazi. Washiriki wa kikao kazi. XXXXXXXXXXXXXX Wataalam wa Sheria na TEHAMA kutoka Taasisi za Haki Jinai wamekutana mjini Morogoro ili kuandaa mahitaji ya mfumo wa kabadilishana taarifa miongoni mwa Taasisi hizo nchini. Kikao hicho  kimeandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kikiwa na lengo la kuwezesha taasisi za Haki jinai kuwa na mifumo thabiti inayosomana na kufanikisha maamuzi yanayofanyika kwenye mfumo wa Haki jinai kuwa yenye tija. Aidha, kikao hicho kitawezesha kujua mifumo iliyopo katika Taasisi ya kuwezesha kubadilishana taarifa, kujua taarifa ambazo zinahitajika kubadilishana baina ya Taasisi na kukubaliana maeneo ya kuhifadhi mifumo itakayowezesha kubadilishana taarifa. Taasisi zinazoshiriki kwenye kikao hicho ni Mahakama, Polisi, Magereza, Mkemia Mkuu,  Wizara ya mambo ya Ndani, Uhamiaji, Ustawi wa Jamii, TAKUKURU, Ofisi ya

WANANCHI KUNUFAIKA NA UTAJIRI ASILI NA MALIASILIA ZA NCHI- MHE. PINDA

Image
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akifungua kikao kazi cha kuandaa mkakati jumuishi wa utekelezaji wa Sheria za Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 449 na Sheria ya Mapatano na Majadiliano kuhusu masharti hasi   katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 450. Mkurugenzi wa Kitengo Cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Bi. Neema Mwanga  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akufungua kikao kazi   Washiriki wa kikao kazi. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXX Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amewataka washiriki wa kikao kazi Cha kuandaa mkakati jumuishi wa utekelezaji wa Sheria za Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 449 na Sheria ya Mapatano na Majadiliano kuhusu masharti hasi   katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 450, kuandaa mkakati imara ambao utakuwa na dira

WAZIRI NDUMBARO AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA WIZARA JIJINI DODOMA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akitoa maelekezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma.   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha wataalam wa ujenzi na menejimenti ya wizara ili kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha wataalam wa ujenzi na menejimenti ya wizara ili kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria linaloendelea kujengwa Mtumba, jijini Dodoma. Dkt. Ndumbaro amefanya ukaguzi huo Leo Novemba 04, 2022 baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati ya ujenzi ya Wizara na Kwa Mkandaras

WATUMISHI KATIBA NA SHERIA WATAKIWA KUCHAPA KAZI NA KUZINGATIA UADILIFU NA NIDHAMU

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na watumishi wa Wizara hiyo. Viongozi waliowahi kuongoza katika wizara hiyo kwa nafasi mbalimbali wakikabidhiwa zawadi. Watumishi wastaafu wakikabidhiwa zawadi. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kuelewa majukumu waliyonayo si lelemama hivyo wayatekeleze kwa kuzingatia uchapakazi, uadilifu, nidhamu na kufanya kazi kama timu ili kuweza kuleta matokeo mazuri ya kazi zao. Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Novemba 3, 2022 jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na watumishi hao kabla ya hafla ya kuwaaga viongozi na watumishi wa Wizara hiyo waliostaafu. Waziri Ndumbaro amesema ‘’Wizara hii ni wizara kubwa na nyeti kwa sababu imeshikilia Katiba ya nchi, pia inashughulika na sheria ambayo ndiyo kila kitu katika utawala wa nchi’’ Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa ‘’Nataka muelewe kwamba jukumu tulilonalo si lelemama tutaweza kulitekeleza tukizingatia uchapaka

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UELEWA MAAFISA VIUNGO WA HAKI ZA BINADAMU YAFUNGWA

Image
  XXXXXXXXXXXXX Mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa Maafisa Viungo wa Haki za Binadamu kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali yaliyokuwa yanafanyika Jijini Arusha tangu tarehe 1 Novemba, 2022 yamefungwa leo Novemba 03, 2022 na ndugu Wankyo Simon Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria. Katika hotuba yake ndugu Wankyo amesema “kwa ujumla mafunzo yaliyotolewa yana faida kubwa kwa Taifa hasa eneo la haki za binadamu na hivyo sisi tuliobahatika kuhudhuria tukayatumie vizuri katika kuboresha taarifa za haki za binadamu tunazotoa mara kwa mara.  Aidha, ameishukuru Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki kwa kukubali ombi la Wizara ya Katiba na Sheria kuongeza awamu nne za mafunzo kama haya kwa mwaka.  

CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI CHATAKIWA KUJITANGAZA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na viongozi wa Chama cha Mawakili wa Serikali walipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma.  Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa muda wa Chama Cha Mawakili wa Serikali walipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma Leo Novemba 03, 2022. Katika mazungumzo hayo Waziri Ndumbaro amewataka viongozi hao kujitangaza ili waweze kujulikana na thamani yao kuonekana na kuwa kubwa. Dkt. Ndumbaro amesema " tunakazi ya kufanya kujitangaza ili kuonekana na wanachama waone faida ya Chama. Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa " Nyie kama Chama Cha Mawakili mhakikishe Sekta ya sheria inakuwa juu kupitia kujitangaza kwenu" Mbali na hayo Dkt. Ndumbaro aliwaasa viongozi wa Chama hicho kupigania maslahi na stahiki za wanachama wao ili waone faida ya kuwepo Kwa Chama hicho. Vilevile Dkt. Ndumbaro aliwaagiza viongozi hao kuwa

KULINDA HAKI ZA BINADAMU NI KULETA USTAWI WA TAIFA: DKT. NDUMBARO

Image
 XXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema nchi inapolinda haki za binadamu kwa mtu mmoja mmoja, makundi na jamii kwa ujumla kwa kuzingatia Katiba ya nchi kunaleta ustawi wa Taifa na maendeleo ya watu. Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa Maafisa Viungo wa Haki za Binadamu kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali juu ya mfumo wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu leo tarehe 1 Novemba, 2022 Jijini Arusha. Katika hotuba yake Dkt. Ndumbaro amesema “Serikali itaendelea kuheshimu na kulinda misingi ya demokrasia na haki za binadamu kwa ajili ya ustawi wa Taifa kwa kuzingatia Katiba ya nchi na Serikali itachukua hatua za kuheshimu na kuzingatia mifumo ya kulinda haki za binadamu” Aidha, Dkt. Ndumbaro amesisitiza kwamba kulindwa kwa haki za binadamu huwafanya wananchi waishi kwa amani na kuwawezesha kutekeleza malengo yao ya kimaisha na kupata maendeleo chanya. Akiongelea lengo la mafunzo hayo Dkt.