CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI CHATAKIWA KUJITANGAZA


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na viongozi wa Chama cha Mawakili wa Serikali walipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma.





 Picha ya pamoja.

XXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa muda wa Chama Cha Mawakili wa Serikali walipomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma Leo Novemba 03, 2022.

Katika mazungumzo hayo Waziri Ndumbaro amewataka viongozi hao kujitangaza ili waweze kujulikana na thamani yao kuonekana na kuwa kubwa.

Dkt. Ndumbaro amesema " tunakazi ya kufanya kujitangaza ili kuonekana na wanachama waone faida ya Chama.

Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa " Nyie kama Chama Cha Mawakili mhakikishe Sekta ya sheria inakuwa juu kupitia kujitangaza kwenu"

Mbali na hayo Dkt. Ndumbaro aliwaasa viongozi wa Chama hicho kupigania maslahi na stahiki za wanachama wao ili waone faida ya kuwepo Kwa Chama hicho.

Vilevile Dkt. Ndumbaro aliwaagiza viongozi hao kuwaambia wanachama wao kutoruhusu mkataba wowote kupita bila kufanyiwa uhakiki Kwani kesi nyingi zinazaliwa na mikataba isiyo sahihi. 

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amewataka viongozi hao na wanachama wao kusaidia katika zoezi la utoaji wa Msaada wa Kisheria, utoaji wa Elimu ya Katiba na kutoa maoni yao Katika sheria ya ndoa.

Awali akielezea lengo la kumtembelea Waziri Ndumbaro Rais wa Chama hicho Bw. Michael Lwena amesema wao kama Chama Cha Mawakili wa Serikali wapo tayari kupokea maelekezo na kushirikiana na Wizara Katika kuiendeleza Sekta ya sheria.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA