DKT. NDUMBARO AIASA JAMII KUACHA VITENDO VYA UKATILI


Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya akifungua kikao cha mtandao wa masuala ya familia kuhusu upatikanaji wa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Meza kuu.

Washiriki.

Picha ya pamoja.

 XXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiasa jamii kuachana na Vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya kwa niaba ya Dkt. Ndumbaro katika ufunguzi wa kikao cha mtandao wa masuala ya familia na Wadau kutoka  Wizara  mbalimbali kuhusu upatikanaji wa sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika Novemba 16, 2022 mjini Morogoro.

Amesema, "kama tunataka kuwa na jamii imara, ni lazima sote tuungane na kupinga Vitendo vyovyote vya ukatili"

Vilevile, katika hotuba yake Dkt. Ndumbaro amewataka Wadau hao kusaidiana na serikali kutoa elimu na kuendelea kukemea vitendo vya ukatili kwani hata kama kutakuwa na sheria nzuri, lakini jamii haina uelewa wa masuala ya ukatili wa kijinsia mapigano ya ukatili wa kijinsia hayatafanikiwa ipasavyo.

Dkt. Ndumbaro, pia alitoa rai kuwa mapendekezo yanayotolewa na Wadau yachukuliwe kwa makini na kuwasilishwa kwa Waziri wa Katiba na Sheria ili aweze kuyashughulikia kwa  mujibu wa sheria.

Akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao hicho Mwenyekiti wa mtandao wa familia Wakili Utti Mwang'amba amesema mtandao wa masuala ya familia uliundwa ili kuhakikisha ukatili wa kijinsia ambao umeshamiri kwenye jamii unatokomezwa na kuwa na jamii iliyo salama.

Ameongeza kuwa kutungwa kwa sheria hiyo kutasaidia jamii kuepukana na vitendo hivyo kwani adhabu zitakazotolewa zinaweza kuleta uoga wa kufanya vitendo hivyo.

Kikao hicho kimeandaliwa ili kuandaa na kupeleka mapendekezo Serikalini ya wataalam kutoka Serikalini na taasisi binafsi juu ya hoja ya kuwa na sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA