DKT. NDUMBARO ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

 XXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro anashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Balaclava, nchini Mauritius kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba, 2022.

Mkutano huo umefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Pravind Kumar Jugnauth.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali katika sekta ya sheria yakiwemo masuala ya upatikanaji haki, Haki za Binadamu, matumizi ya akili bandia katika mifumo ya Mahakama, umuhimu wa sekta ya sheria katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Mambo mengine yanayotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Urejeshwaji wa Wahalifu, Mikataba ya Uwekezaji, Hatua zilizochokuliwa na Nchi Wanachama katika maeneo mbalimbali yakiwemo Mapambano dhidi ya Rushwa, Sheria za Kudhibiti uhalifu wa mtandao, Ushirikiano katika masuala ya Jinai na Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala na  wajibu wa Vyombo vya Habari katika kutekeleza Haki ya Kutoa Maoni.

Mkutano huo unahudhuriwa na Mataifa zaidi ya 30 kutoka katika Wanachama wa Jumuiya ya Madola Duniani.

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA