JIUNGENI NA CHAMA CHA MAWAKILI CHA AFRIKA MASHARIKI- MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


 
XXXXXXXXXXXXX

Rais Samia Suluhu Hassan  amewataka Mawakili  nchini kujiunga na Chama Cha Mawakili Cha Afrika Mashariki (East Africa Law Society).

Mheshimiwa Rais ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa  Chama Cha Mawakili Cha Afrika Mashariki tarehe 24 Novemba, 2022 Jijini Arusha .

Akiongea kwenye kikao hicho Mhe. Rais amesema "Afrika Mashariki Sasa ni wamoja tunafanya kazi kwa kushirikiana, na nyinyi shirikianeni kutatua kesi mbalimbali ndani ya Jumuiya yetu na nje ya Jumuiya, kuweni wamoja na imara  katika kujenga Chama chenu" 

Aidha Mheshimiwa Rais amewaomba Mawakili  kuwakaribisha Mawakili kutoka DRC Congo , ambao wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi karibuni. 

Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda  ambaye alimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  amesema " ni fursa kwa Mawakili   wetu kufanya kazi ndani ya Afrika Mashariki kwasababu watajijengea  uwezo na kujifunza mambo mengi kutoka kwa wengine, nafasi kama hizi zinakufanya ujue mambo mbalimbali ya kisheria pamoja kutambulika kimataifa". 

Pia Mhe. Pindaa amewataka Mawakili wa Chama hicho kushirikiana  katika kutatua kesi mbalimbali.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA