JUKUMU LA KUHIFADHI WAKIMBIZI SIYO JEPESI HASA KWA NCHI WENYEJI- MHE PINDA
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kujadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi na Wahamiaji kilichofanyika jijini, Arusha.Washiriki wa kikao.
Picha ya pamoja.
XXXXXXXXXXXXXXXXXX
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amesema kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokimbia makazi yao jukumu la kuhifadhi Wakimbizi ni jukumu zito hasa kwa nchi inayopokea Wakimbizi.
Mhe. Pinda ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kujadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi na Wahamiaji kilichofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 18 Novemba, 2022 jijini Arusha.
Katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema " Serikali imekuwa ikihifadhi Wakimbizi kwa muda mrefu, hivyo inatambua mchango mkubwa wa wadau wa masuala ya Wakimbizi katika nyanja zote".
Aidha, Mhe. Pinda amesema "kama mnavyofahamu Wakimbizi wengi wanahifadhiwa katika nchi zinazoendelea na Tanzania tuna Wakimbizi zaidi ya 256,000 ambao wamehifadhiwa kwenye kambi mbali mbali nchini".
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Huduma Kwa Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu, Sudi Mwakibasi amesema Serikali imekuwa ikitoa ushirikiano mzuri na wadau mbalimbali katika kuhudumia Wakimbizi na hii ni kwasababu tuna historia nzuri ya kupokea Wakimbizi kutoka nchi mbalimbali na wanaishi kwa amani na utulivu.
Comments
Post a Comment