MAFUNZO YA KUWAJENGEA UELEWA MAAFISA VIUNGO WA HAKI ZA BINADAMU YAFUNGWA


 

XXXXXXXXXXXXX

Mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa Maafisa Viungo wa Haki za Binadamu kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali yaliyokuwa yanafanyika Jijini Arusha tangu tarehe 1 Novemba, 2022 yamefungwa leo Novemba 03, 2022 na ndugu Wankyo Simon Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria.

Katika hotuba yake ndugu Wankyo amesema “kwa ujumla mafunzo yaliyotolewa yana faida kubwa kwa Taifa hasa eneo la haki za binadamu na hivyo sisi tuliobahatika kuhudhuria tukayatumie vizuri katika kuboresha taarifa za haki za binadamu tunazotoa mara kwa mara. 

Aidha, ameishukuru Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki kwa kukubali ombi la Wizara ya Katiba na Sheria kuongeza awamu nne za mafunzo kama haya kwa mwaka.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA