TAASISI ZA HAKI JINAI ZAANDAA MFUMO WA KUBADILISHANA TAARIFA


Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Ernest Mbuna akitoa mada katika kikao cha maandalizi ya mfumo wa Haki Jinai.
Washiriki wa kikao kazi.

Washiriki wa kikao kazi.
XXXXXXXXXXXXXX

Wataalam wa Sheria na TEHAMA kutoka Taasisi za Haki Jinai wamekutana mjini Morogoro ili kuandaa mahitaji ya mfumo wa kabadilishana taarifa miongoni mwa Taasisi hizo nchini.

Kikao hicho  kimeandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kikiwa na lengo la kuwezesha taasisi za Haki jinai kuwa na mifumo thabiti inayosomana na kufanikisha maamuzi yanayofanyika kwenye mfumo wa Haki jinai kuwa yenye tija.

Aidha, kikao hicho kitawezesha kujua mifumo iliyopo katika Taasisi ya kuwezesha kubadilishana taarifa, kujua taarifa ambazo zinahitajika kubadilishana baina ya Taasisi na kukubaliana maeneo ya kuhifadhi mifumo itakayowezesha kubadilishana taarifa.

Taasisi zinazoshiriki kwenye kikao hicho ni Mahakama, Polisi, Magereza, Mkemia Mkuu,  Wizara ya mambo ya Ndani, Uhamiaji, Ustawi wa Jamii, TAKUKURU, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, TAWA, Kitengo Cha Kudhibiti Fedha Haramu Tanzania na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA