WANANCHI KUNUFAIKA NA UTAJIRI ASILI NA MALIASILIA ZA NCHI- MHE. PINDA


 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akifungua kikao kazi cha kuandaa mkakati jumuishi wa utekelezaji wa Sheria za Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 449 na Sheria ya Mapatano na Majadiliano kuhusu masharti hasi   katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 450.


Mkurugenzi wa Kitengo Cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Bi. Neema Mwanga Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda akufungua kikao kazi 


Washiriki wa kikao kazi.


Picha ya pamoja.

XXXXXXXXXXXX

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda amewataka washiriki wa kikao kazi Cha kuandaa mkakati jumuishi wa utekelezaji wa Sheria za Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 449 na Sheria ya Mapatano na Majadiliano kuhusu masharti hasi   katika Mikataba ya Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi sura 450, kuandaa mkakati imara ambao utakuwa na dira ya kuwa na taifa ambalo wananchi wake wanapata haki ya kunufaika na Utajiri Asili na Maliasilia zake.

Mhe. Pinda ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu cha kuandaa mkakati huo leo Novemba 8, 2022 Jijini Dodoma.

Mhe. Pinda amesema "tunategemea kikao hiki kije na mkakati wenye dhima ya kuweka mifumo madhubuti kwa mujibu wa Katiba inayowezesha uhifadhi, usimamizi, uvunaji na matumizi ya Utajiri na Maliasilia za nchi kwa manufaa ya wananchi wake".

Zaidi ya hayo Mhe. Pinda  ameongeza kuwa mkakati utakaoandaliwa uweke misingi mikuu inayoakisi sera na mipango mbalimbali ya Taifa ya sasa na baadae, ugatuzi wa mifumo ya uendeshaji na usimamizi, uhuru, ushirikiano, uwajibikaji na kuongeza kasi Katika maendeleo ya nchi.

Vilevile Mhe. Pinda ameongeza kuwa ni wajibu wa Serikali na vyombo vyote kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu wa pamoja Katika kusimamia Utajiri Asili na Maliasilia za nchi kwa kuzingatia haki za kiuchumi na kijamii.

Akimkaribisha Mhe. Pinda, Mkurugenzi wa Kitengo Cha Uangalizi wa Utajiri wa Asili na Maliasilia za Nchi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Bi. Neema Mwanga amesema mkakati huo unahuishwa kwa upana ili uwe jumuishi na kuwezesha uratibu wa sekta zote ambazo zimetajwa na sheria unatekelezwa.

Bi. Neema aliongeza kuwa kutungwa kwa sheria za Mamlaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri na Maliasilia za nchi kumewezesha kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa na mifumo sahihi ya usimamizi imewekwa.

Akitoa neno la shukran kwa Naibu Waziri baada ya kufungua kikao kazi hicho Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma Dkt. Aron Kinunda ameahidi kwa niaba ya washiriki wengine kuwa kwa siku tatu watakazokuwa wanaandaa mkakati huo watahakikisha wanatoka na kitu chenye tija Kwa nchi na wananchi wake na kuweza kusaidia Taifa.

Kikao kazi hicho kimejumuisha wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Uvuvi, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Nishati, TAMISEMI, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, Chuo Kikuu Cha Dodoma na Chuo Cha Uongozi.

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA