WAZIRI NDUMBARO AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA WIZARA JIJINI DODOMA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akitoa maelekezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma.
 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha wataalam wa ujenzi na menejimenti ya wizara ili kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha wataalam wa ujenzi na menejimenti ya wizara ili kupata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba, jijini Dodoma.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita la Wizara ya Katiba na Sheria linaloendelea kujengwa Mtumba, jijini Dodoma.

Dkt. Ndumbaro amefanya ukaguzi huo Leo Novemba 04, 2022 baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati ya ujenzi ya Wizara na Kwa Mkandarasi.

Katika taarifa hizo kuna changamoto zilizoonekana kukwamisha kukamilika kwa ujenzi katika muda wa awali na hivyo Mkandarasi kuomba kuongezewa muda zaidi.

Dkt. Ndumbaro ameelekeza changamoto hizo zitatuliwe ikiwemo kuongeza vibarua na muda wa kufanya kazi na pia amesisitiza taratibu za malipo zifanyike Kwa wakati ili kuwezesha malipo kutoka mapema na kutokwamisha ujenzi.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amemtaka Mkandarasi kuagiza malighafi mapema na kuepuka changamoto ya kupotea kwa malighafi hizo sokoni na kuchelewesha ujenzi.

Katika mkataba wa awali ujenzi huo ulipaswa kukamilika mwezi Septemba 2022, Lakini baada ya kuongezewa muda unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2023.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA