WAZIRI NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA KITUO JUMUISHI


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Khatibu Kazungu akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza, Novemba 29, 2022. 


XXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo Jumuishi cha Sheria Mkoani Mwanza leo Novemba 29, 2022. 

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Patience Ntwina.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro amepongeza jitihada hizo na ushirikiano uliooneshwa kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa  kufanikisha ndoto hiyo ya kuwa na Kituo Jumuishi.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa ujenzi huo utawezesha kupunguza na kuondoa gharama kwa wateja kwa kuwa utawawezesha kupata huduma sehemu moja.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA