WIZARA YA KATIBA NA SHERIA IMEJIPANGA KUBORESHA MIUNDOMBIMU YA MAHAKAMA

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same.  

 



XXXXXXXXXXXXXXXX


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Geophrey Mizengo Pinda amesema  Wizara imejipanga kuhakikisha miundombinu ya Mahakama inakuwa bora.

Mhe. Pinda amesema hayo jana tarehe 15 Novemba, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya ya Mwanga na Same.

Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Pinda amesema "Serikali  yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan   inahakikisha mazingira ya utoaji haki katika Mahakama zetu yanakuwa bora na rafiki, na tayari kwa mwaka huu tunashuhudia Mahakama mbalimbali zikijemgwa,  tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais."

Aidha, Jaji Mkuu Mheshimiwa Prof. Ibrahimu Juma amesema Mahakama imejiwekea mkakati kuhakikisha  inaendelea kujenga majengo ya Mahakama kwa zile Wilaya ambazo majengo yao yamechakaa ili kuhakikisha wanasogeza  huduma ya haki kwa Wananchi.

Akiongelea gharama za ujenzi huo, Mheshimiwa Jaji Mkuu amesema majengo hayo yamejengwa kwa fedha za ndani zinazotokana na Kodi za Wananchi na kusisitiza utunzwaji wa majengo hayo.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA