WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KUANDAA MPANGO KAZI WA UFUATILIAJI NA TATHIMINI.


 XXXXXXXXXXX
Wizara ya Katiba na Sheria inaandaa Mpango Kazi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa mwaka wa shughuli zote za Wizara. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera, Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini ndugu Emmanuel Mayeji kwenye kikao kazi cha siku tano kinachofanyika kuanzia tarehe 28 Novemba hadi 2 Desemba 2022 mjini Morogoro. 

Ndugu Mayeji  amesema " kakao hiki  kina malengo makuu mawili , Moja  kujadili namna ya kuwa na mfumo thabiti wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni , Miongozo na Mipango inayosimamiwa"

Mbili kuwa na mfumo  thabiti wa utoaji wa taarifa  za utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kuzingatia takwimu sahihi za mafanikio na changamoto zilizojitokeza pamoja na kuwa na  mkakati wa kutatua changamoto zilizojitikeza wakati wa utekelezaji" .

Aidha kikao kazi hicho kinahudhuriwa na  maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.


Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA