DKT. DAMAS DUMBARO AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU
XXXXXXXXXXXXX
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amezindua maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Bindamu kitaifa.
Maadhimisho hayo yamezinduliwa tarehe 6 Desemba, 2022 katika viwanja vya Nyerere Square vilivyopo katikati ya mji, jijini Dodoma.
Akiongea kwenye Uzinduzi huo Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema "Maadhimisho haya yameanza mwaka 2016 kwa lengo la kuwa na siku ya kimataifa ya kupambana na Rushwa pamoja na siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu ili kuwaelimisha wananchi namna ya kupiga vita rushwa na pia juu ya masuala ya Haki za Binadamu."
Pia Dkt. Ndumbaro amesema "Jukumu kubwa la Serikali yetu ni kuwaletea Wananchi maendeleo, hivyo Usimamizi wa Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Uwazi na mapambano dhidi ya rushwa ni masuala endelevu kwa kuwa ni msingi wa utoaji huduma bora kwa Umma."
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema _"Maadili, Haki za Binadamu, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu la pamoja kati ya Serikali, Wananchi na Wadau Wengine"._
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bi. Neema Mwakalyelye amesema "kupiga vita Rushwa ni jukumu letu sote, rushwa inarudisha maendeleo nyuma."
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Bindamu Bi. Nkasori Sarakikya ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria amesema "Wizara imejipanga kutoa elimu na Huduma Kwa Umma kuhusu Haki za Binadamu na Huduma ya Msaada wa Kisheria."
Comments
Post a Comment