DKT. NDUMBARO AKUTANA NA MAAFISA KUTOKA UBALOZI WA UINGEREZA


 

XXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini; Dkt. Zabdiel Kimambo -Mshauri wa Utawala, Bw. Laurence Wilkes, Mshauri wa Masuala ya Utawala na Siasa, na Bi. Allanna Inserra, Mshauri wa Masuala ya Siasa tarehe 14 Desemba, 2022 katika Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo ushirikiano baina ya Serikali na Asasi za Kiraia na utekelezaji wa miradi ambayo inafadhiliwa na Uingereza kupitia Asasi mbalimbali hapa nchini.

Dkt. Ndumbaro ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuwa na ushirikiano na uhusiano mzuri na Asasi za Kiraia hususan katika upatikanaji wa maoni katika sheria mbalimbali zinazohitaji kufanyiwa marekebisho. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Casmir Kyuki na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje.

Kwa upande wake Bw. Wilkes, aliahidi kuwa Ubalozi wa Uingereza utaendeleza ushirikiano na Serikali na utakuwa tayari kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali hususan katika masuala ya upatikanaji haki.


Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA