DKT. NDUMBARO ASHIRIKI HAFLA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU WA KENYA





XXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax katika Hafla ya maadhimisho ya miaka ya 58 ya Uhuru wa Taifa la Kenya yaliyofanyika tarehe 12/12/2022, Jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahaman Kinana, Amidi wa Mabalozi wa mataifa mbalimbali Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui.

Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya, ni fursa pekee ya kuangalia mahusiano baina ya nchi hizo mbili ambapo siku zote yamezidi kuimarika kama yalivyoasisiwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Aidha, Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa pamoja na kwamba mahusiano katika Nyanja za Biashara yamezidi kuimarika zinahitajika jitihada zaidi na kutoa rai kwa wafanyabiashara kuendelea kuvumbua fursa zaidi zainazopatikana katika nchi hizo mbili.

Mwenyeji wa Hafla hiyo, Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Mhe. Isaac Njenga, amesisitiza kuwa Kenya itandelea kuimarisha Sera yake ya diplomasia ya uchumi na kuendelea kuhusisha mipango mikakati mbalimbali ya nchi zao ili kuendana na falsafa hiyo.

 

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA