RAIS SAMIA ARIDHIA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 77 WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA WA HAKI ZA BINADAMU NA WATU.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu alipofika Ikule ya DSM leo 30/01/2023. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Ndumbaro na viongozi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na asasi za kiraia za watetezi wa haki za binadamu. XXXXXXXXXXX Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu la kuitaka nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 77 utakaojumuisha nchi wanachama wa kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Rai...