Posts

Showing posts from January, 2023

RAIS SAMIA ARIDHIA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 77 WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA WA HAKI ZA BINADAMU NA WATU.

Image
  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu alipofika Ikule ya DSM leo 30/01/2023. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Ndumbaro na viongozi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na asasi za kiraia za watetezi wa haki za binadamu. XXXXXXXXXXX Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu la kuitaka nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 77 utakaojumuisha nchi wanachama wa kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Rais Sa

NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MASUALA YA AJIRA NA SHERIA ZA KAZI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akionesha kitabu alichokizindua chenye kurasa Zaidi ya 900. Kulia kwake ni mwandishi wa kitabu hicho Wakili Ally Kileo na kushoto ni Prof. Chris Peter Maina. Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na mwandishi wa kitabu hicho Wakili Ally Kileo pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa kitabu hicho. Wakili Ally Kileo ikimkabidhi Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro zawadi mara baada ya kukamilisha kazi ya uzinduzi wa kitabu hicho. XXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezindua kitabu cha masuala ya ajira na sheria za kazi chenye kurasa zaidi ya Mia Tisa jijini Dar es salaam na kuwataka watanzania wengine kujikita katika kuandika vitabu hasa vyenye uchambuzi wa kisheria ambavyo vitawaongezea uelewa watanzania juu ya sheria zao na haki wanazostahili. Waziri Ndumbaro ameyasema hayo usiku wa jana Tarehe 25/01/2023 alipoalikwa kama Mgeni Ras

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUFANYIKA NCHI NZIMA: DKT. KAZUNGU

Image
  Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akifungua kikao kazi cha wajumbe wa Kamati ya maandilizi ya kampeni ya Msaada wa Kisheria tarehe 24 Januari, 2023 Jijini Dodoma. Wajumbe wa Kamati wakimsikiliza mgeni rasmi Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha kamati hiyo. Picha ya pamoja. XXXXXXXXXXX Serikali imejipanga kufanya kampeni ya Msaada wa Kisheria nchi nzima itayolenga kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na sheria kwa watanzania wote. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu alipokuwa akifungua kikao kazi cha wajumbe wa Kamati ya maandilizi ya kampeni hiyo tarehe 24 Januari, 2023 Jijini Dodoma. “Wananchi wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kisheria hali inayopelekea wengi wao kukosa haki zao, kutokuzipata kwa wakati au kuzipata kwa gharama kubwa sana.” Alisema Dkt. Kazungu. Kampeni hiyo ambayo imepewa jina la _Mama Samia Legal

MAONESHO YA WIKI YA SHERIA: WATATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA MBADALA WAANZA KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI.

Image
  Wizara ya Katiba na Sheria imeanza kuwasajili watatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, upatanishi, majadiliano na ufanyaji maridhiano kwa kupitia mfumo wa kielektroniki ulioundwa mwaka jana na kuanza kutumika rasmi Juni, 2022 kwa lengo la kurahisisha hatua zinazotakiwa kutekelezwa wakati wa usajili. Taarifa hiyo imetolewa na Wakili wa Serikali Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bwana  Elia Athanas alipokuwa anamwelezea Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria kabla ya uzinduzi rasmi wa maonesho haya ya Wiki ya Sheria. Wakili Athanas alisema mfumo huu umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wanaojihusisha na kazi za utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kwani hivi sasa hawalazimiki tena kusafiri hadi Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha maombi yao ya usajili  bali kwa kutumia kompyuta yenye internet wanaweza kutuma nyaraka na kuwasilisha maombi yao. “Mheshimiwa Mgeni Rasmi, kabla ya kuanza