XXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro amepongezwa kwa kusimamia ukamilishwaji wa uandishi na uchapishaji wa Kitabu cha miaka 60 ya Uhuru na Sekta ya Sheria tulipotoka,tulipo na tunapokwenda tangu mwaka (1961 - 2021). Kitabu hicho kimeweka historia na kumbukumbu ya miaka 60 kinatoa kipimo tosha cha maendeleo katika taasisi mbalimbali za serikali kwa miongo yote 6 tangu uhuru ikiwa ni umri wa mtumishi wa Serikali kustaafu. Akitoa pongezi hizo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa kitabu hicho leo Februari 7,2023 jijini Dodoma,aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika Serikali ya awamu ya tano na sasa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa historia sio habari ya mambo yaliyopitwa bali ni mambo yaliyopita ambayo yanamwangwi kwa mambo yaliyopo kwa sasa. "Historia ni habari iliyopita ambayo yanaakisi mambo ya sasa ni chemichemi ambayo jamii iliyaishi,inayaishi na kurithisha kwa vizazi na vizazi kw...