DKT. NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MIAKA 60 YA UHURU NA SEKTA YA SHERIA
XXXXXXXXXXXXXX
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Damas
Ndumbaro amepongezwa kwa kusimamia ukamilishwaji wa uandishi na uchapishaji wa
Kitabu cha miaka 60 ya Uhuru na Sekta ya Sheria tulipotoka,tulipo na
tunapokwenda tangu mwaka (1961 - 2021).
Kitabu hicho kimeweka historia na kumbukumbu ya miaka 60 kinatoa kipimo tosha cha maendeleo katika taasisi mbalimbali za serikali kwa miongo yote 6 tangu uhuru ikiwa ni umri wa mtumishi wa Serikali kustaafu.
Akitoa pongezi hizo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa kitabu hicho leo Februari 7,2023 jijini Dodoma,aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika Serikali ya awamu ya tano na sasa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa historia sio habari ya mambo yaliyopitwa bali ni mambo yaliyopita ambayo yanamwangwi kwa mambo yaliyopo kwa sasa.
"Historia ni habari iliyopita ambayo yanaakisi mambo ya sasa ni chemichemi ambayo jamii iliyaishi,inayaishi na kurithisha kwa vizazi na vizazi kwa kuwekwa katika vitabu,"amesema Pro.Kabudi
Prof.Kabudi amesema kwa miaka mingi historia ya Tanzania imekuwa ya simulizi badala ya kuandikwa ,hivyo kupitia kitabu hicho kitasaidia watu wengi kusoma na kuelewa kiundani kuhusu nchi ilipotoka,ilipo na kupata tathmini inapoelekea na kufanya vijana wengi wa sasa na baadae kujua jinsi nchi ilivyopiga hatua za maendeleo.
"Kitabu hiki kitasaidia kuzikabili changamoto zilizopo kwa sasa kwa kuyarejea mambo ya zamani ili kupata njia ya kwenda mbele kufikia mafanikio kijamii na kitaifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Prof,Sifuni Mchome amesema kuwa kitabu hicho kitasaidia kupima nchi yote ilipotoka na inapokwenda na ili kufaanikisha hilo kila baada ya miaka mitano kitabu hicho kinakuwa kinachapishwa ili kuongeza historia zinazoendelea kutokea ndani ya miaka hiyo.
"Kitabu hiki kitakuwa kinatoka kwa Edition hii ya kwanza ya miaka 60 na kila baada ya miaka mitano itatoka Edition ya pili nia na mazumuni ni kuendelea kukumbusha historia ya nchi yetu kwa vizazi na vizazi,"amesema Prof.Mchome
Comments
Post a Comment