“ARUSHA NI MJI WA KIMATAIFA WA SHERIA” - NDUMBARO

Waliokaa ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro akiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari Mhe. Jaji Graciela Gatti Santana pamoja Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama(Mb), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul na Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo na viongozi wengine wa Wizara na Mahakama ya Kimbari katika picha ya pamoja. XXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe, Lusajo Mwakabuku na Nkasori Sarakikya - WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (UN-International Residual Mechanism for Criminal Tribunals), iliyopo Arusha Jaji Graciela Gatti Santana leo tarehe 28 machi 2023 jijini Dodoma. Akiongea kwenye kikao hicho...