“ARUSHA NI MJI WA KIMATAIFA WA SHERIA” - NDUMBARO
Waliokaa
ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro akiwa na Rais wa Mahakama
ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari Mhe. Jaji Graciela Gatti
Santana pamoja Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria, Mhe. Joseph Mhagama(Mb), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline
Gekul na Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo na viongozi wengine
wa Wizara na Mahakama ya Kimbari katika picha ya pamoja.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na George Mwakyembe,
Lusajo Mwakabuku na Nkasori Sarakikya - WKS
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na
Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari
(UN-International Residual Mechanism for Criminal Tribunals), iliyopo Arusha
Jaji Graciela Gatti Santana leo tarehe 28 machi 2023 jijini Dodoma.
Akiongea
kwenye kikao hicho Mhe. Ndumbaro Alieleza umuhimu wa Mahakama ya Kimataifa ya
Mauaji ya Kimbari - Rwanda (UN-International Criminal Tribunal for Rwanda)
kuwepo Arusha huku akiitaja Arusha kuwa ni sehemu sahihi kwa Mahakama hiyo
kutokana na sifa ya Arusha kuwa “Mji wa Kimataifa wa Sheria Afrika”
kunakotokana na Mhakama ya Haki ya Afrika Mashariki pamoja na Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuwepo katika jiji hili la Arusha.
Ndumbaro
alieleza kwamba kutokana na muundo wa Mahakama hiyo ya Kimbari, ni lazima
itafikisha ukomo wake baada ya kesi inazozishughulikia kuisha na kwamba Serikai
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko tayari kuhakikisha kwamba jengo na
maktaba ya Mahakama vitendelea kutumika na kuchangia katika mifumo na Sheria za
kimataifa, hususan Sheria za Kimataifa za Jinai na Haki za Binadamu.
Mheshimiwa
Ndumbaro akaongeza kwa kuwa kazi za Mahakama zinakaribia kuisha basi ni vyema
hayo majengo yakatumika kama chuo cha
kimataifa cha mafunzo ya kisheria. Kufanya hivi kutapelekea utunzaji wa
kumbukumbu nzuri ya utatuzi wa kesi za Mauaji ya Kimbari .
Aidha
Mhe. Ndumbaro amesema kwa kutambua mchango mkubwa uliofanyika katika Mahakama
hiyo Serikali inaomba Maktaba ya Mahakama iliyopo eneo la Lakilaki karibu na
Mahakama hiyo jijini Arusha ifunguliwe
na kuendelea kufanya kazi ili Watanzania pamoja na Wananchi mbalimbali kutoka
Afrika na sehemu zingine za dunia
waweze kujifunza pamoja kujua historia
na kazi kubwa iliyofanywa na
mahakama hiyo.
Naye
Mkurugunzi wa Mashtaka nchini Sylivester Mwakitalu akiwa mmoja wa waalikwa
waliombatana na Mhe. Waziri katika kikao hicho amesema kutokana na kukua kwa
teknolojia, masuala ya uhalifu yamekuwa pia yakiongezeka basi ni vyema kujenga ushirikiano katika
kutoa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali ili kuwajengea uwezo mzuri katika
kukabiliana na uhalifu huo.
Kwa
upande wake Rais wa Mahakama ya Kimbari Mheshimiwa Jaji Graciela Santana
amesema anafurahia kufanya kazi na Tanzania na pia wao wapo tayari kuendelea
kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana na katika masuala mbalimbali hasa ya
kisheria. Jaji Santana amesema Serikali ya Tanzania imekuwa na mchango mkubwa
katika kuhakikisha kesi zote zinasimamiwa kwa utulivu na amani. Aidha, Tanzania
ilikuwa na nafasi ya kipekee wakati wa Mahakama wa UN-UCTR na bado inanafasi
muhimu wakati wa Mahakam ya Kimbari. Hivyo, wataendelea kushirikiana na
Serikali hadi Mahakama hiyo inpohitimisha muda wake.
Jaji Santana pia aliipongeza Serikali kwa
kutaka kuendelea kutumia Mahakama hiyo kwa madhumuni ya kuchangia kweye tasnia
ya Sheria za kimataifa. Kutokana na lengo hilo zuri la serikali, wapo tayari
kufanya majadiliano na Serikali ya Tanzania juu ya Matumizi ya Mahakama hiyo
baada ya kuhitimisha muda wake.
Comments
Post a Comment