DKT. NDUMBARO MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA UDOM

 


Waziri wa Katiba na Sheria  Mh. Damas Ndumbaro  akiwa katika mazungumzo  na Dkt Ines Kajiru  pamoja na timu yake  tarehe 13 machi katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria, Mtumba Jijini Dodoma.  


Dkt Damas Ndumbaro  Waziri wa Katiba na Sheria kwenye picha ya pamoja na Dkt Ines Kajiru  pamoja na timu yake tarehe 13 machi  2023 ofisi  za Wizara, mtumba Jijini Dodoma. 

                                                               xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx 

George Mwakyembe & Lusajo Mwakabuku - WKS

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekubali mwaliko wa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Sheria yanayotarajia kufanyika tarehe 24 Machi 2023 katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa na Amidi wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Ines Kajiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Waziri Ndumbaro leo tarehe 13 Machi 2023 katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria za Mtumba Jijini Dodoma.

Aidha, Dkt Kajiru alimweleza Mhe. Waziri Ndumbaro kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma wapo tayari kushirikiana na Wizara katika masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo kufanya tafiti za kisheria pamoja na ushiriki katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign.

Dkt. Kajiru aliongeza kuwa kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na mambo mengine kingependa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wanyonge wanapata msaada wa kisheria katika kupambania haki zao bila kujali hali ya kipato chao.

Kwa upande wake Mhe. Ndumbaro amesema Wizara ipo tayari kuendeleza ushirikiano katika masuala ya kisheria na kuongeza kwamba Wizara ya Katiba Sheria ni nyumbani kwa kila mtanzania. Waziri Ndumbaro pia akawakaribisha UDOM kushiriki katika Kampeni ya Msaada wa Huduma za Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Campain) kwa lengo la kuweza kuwafikia wananchi wote hasa walioko vijijini.

Katika ujumbe huo Dkt. Kajiru aliambatana na Dkt. Aron Kinunda, Mudiri sheria binafsi, Dkt. Kulwa Gamba, Mudiri sheria za umma pamoja na Bw. Emmanuel Baruti ambaye ni Mratibu wa Kliniki ya Sheria.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA