KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIMWAGIA SIFA MAHAKAMA
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Leonard Magacha( Kulia ) akimwonesha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria (Mb) na Wajumbe wa Kamati hiyo alioambatana nao kwenye ukaguzi wa ukarabati wa jengo la Mahakama liliokuwa likitumika kama ofisi ya Serikali za Mitaa. Tarehe 14 Machi, 2023 Mjini Tabora.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Lusajo Mwakabuku – WKS
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imekagua Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora na kuridhishwa kwa kazi inayofanywa na Mahakama katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya majengo yake.
Mara baada ya ziara hiyo ya siku moja ya ukaguzi wa utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora iliyofanyika tarehe 14 Machi, 2023, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Laurent Kyombo amesema kuwa Mahakama ni moja ya Taasisi inayofanya vizuri katika miradi yake ya ujenzi na hivyo kuwasihi Watumishi wa Mhimili huo kutoa huduma zinazoendana na uzuri wa miundombinu hiyo.
Akimwakilisha
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro katika Ziara hiyo, Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) aliishukuru kamati kwa
pongezi hizo na kuahidi kutolea ufafanuzi kwa maandishi hoja na maswali yote
yaliyoulizwa na Wajumbe wakati wa ziara hiyo na kuahidi kutekeleza ushauri kama
ulivyotolewa na kamati.
Comments
Post a Comment